NINI MAANA YA KIPIGA KITE?

  Maswali ya Biblia

Maana kamili ya “kupiga Kite” ni kutoa pumzi nje, hii huashiria aidha kushangazwa, kupata unafuu au kukata tamaa.

Kwamfano mwanafunzi aliyekuwa anangojea matokeo ya mtihani alioufanya, na wakati anatazama matokeo kwenye orodha ya majina anafanikiwa kuona jina lake katika nafasi za waliofaulu na anajikuta amefaulu basi unaweza kuona anashusha pumzi. (Kitendo hicho cha kushusha pumzi, kana kwamba kapunguza presha ndani yake, ndio kitendo hicho ndicho kinachoitwa kupiga Kite).

Au mtu anayehangaikia kutimiza jambo fulani kwa kipindi cha muda mrefu, na asifanikiwe kwa wakati na kuazimia kujaribu kwa mara moja ya mwisho, kama tumaini lake la mwisho, na wakati anangojea kupata tumaini zuri, ghafla yanakuja matokeo mabaya ya kumvunja moyo, mtu wa namna hiyo pia utaona anashusha pumzi, kuashiria kukata tamaa (kitendo cha namna hiyo pia ni kupiga kite).

Hapo neno “ kupiga” limetumika na sio “kufanya”…kwasababu matendo hayo ya kuvuta pumzi au kutoa, yanatamkwa kwa kuanza na neno “kupiga”..kwamfano “kupiga miayo”, huwezi kusema “kufanya miayo”.

Katika biblia Neno hilo limeonekana mara kadhaa.

Maombolezo 1:11 “Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamaniko yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge”.


Pia,
Maombolezo 1:4 “Njia za Sayuni zaomboleza, Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu; Malango yake yote yamekuwa ukiwa, Makuhani wake hupiga kite; Wanawali wake wanahuzunika; Na yeye mwenyewe huona uchungu”.


Unaweza kusoma pia 9, utaona Neno hilo hilo.Unaweza kusoma pia Maombolezo 1:21, na Zaburi 90:9 , utaona Neno hilo hilo.


Je umemwamini Bwana Yesu?..kumbuka ulimwengu huu unapita na mambo yake yote, miaka yetu inapukutika kama kite, anaanza na matumaini inaishia na huzuni na kukata tamaa, lakini kama tukiwa ndani ya Yesu itaanza na huzuni lakini itaishia na furaha.


Zaburi 90:9
Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako,
Tumetowesha miaka yetu kama kite.
Maran atha!

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Washirikishe na wengine habari hizi njema Kwa kushea, au wasiliana nasi kwa namba hii 255693036618,255789001312

LEAVE A COMMENT