Melkizedeki ni nani katika maandiko je ni Malaika au Mungu?.

Biblia kwa kina No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Melkizedeki kama tunavyosoma katika maandiko si mwingine bali ni Kristo Yesu yaani Mungu!, kwa namna gani? Tutakwenda kutazama kwa undani zaidi ili kulidhibitisha jambo hili.

Maandiko yanatuambia….

1 Timotheo 3:16
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.

Ikiwa na maana kuzitambua ama kumuelewa Mungu si jambo la kawaida kama tunavyodhani la!, Mungu kaviweka vitu vinavyomhusu yeye katika SIRI kubwa sana kwa namna ya kawaida pasipo kufunuliwa na Bwana hakuna awezae kujua.

Sasa ni kwa namna gani Huyu Melkizedeki ndio alikuwa Mungu mwenyewe? Jambo hili Bwana Yesu alipowaambia Mafarisayo wakataka kumpiga mawe walishindwa kuelewa tusome….

Yohana 8:57 “Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?

58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko”.

Unaona hapo? Katika mstari huo wa 58 anasema “…..yeye Ibrahimu asijakuwako,mimi niko”

Turejee hapa kidogo pia tuone jambo…

Kutoka 3:14
Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu.

Neno hili kipindi anamtuma pia Musa alisema vivyo hivyo kama aliposema na Wayahudi kuwa “….Mimi niko”

Sasa kwa namna gani alikuwepo hapa ndipo panaleta mkanganyiko mkubwa watu wasio wa Kristo na baadhi ya Wakristo wanashindwa kupambanua hapa wakisoma.

Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Sasa Yesu mwenyewe ndio Neno ikionesha kwamba kumbe Yesu alikuwa kabla ya kitu chochote kuwepo hapa ulimwengu na sehemu zingine zote yeye alikuwepo “hakika siri ya uungu ni kuu sana Haleluya “.

Sasa kwa Lugha ya asili yaani Kigiriki iliyotumika kuandika Biblia Kwa Kigiriki Neno ni LOGOS ikiwa na maana “WAZO WALA MUNGU ” au mpango na makusudio ya Mungu.

Sasa Neno hili tunalisoma lengo lake/kusudi lake kuu ni nini??

1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya NENO LA UZIMA;

2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);

3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo”

Kumbe Neno hili limebeba uzima Haleluya!!, na uzima huo ni wetu sisi ambao Mungu ameukusudia toka kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu(yaani kabla hata hajatuumba) “hakika Mungu hakuna awezae kumchunguza na kuyajua makusudio yake.”

Mtume Yohana anasema “lile tulilolisikia..” maana yake walikuwa wakilisikia tu toka zamani kupitia Manabii kama Isaya, Yeremia nk. Baada ya muda Sasa ulipofika wakati wake wa kutimililka na kufanya ukombozi kwetu wa kutuweka huru ndio likadhirika kwa macho likawa linashikia kwa mikono na kulipapasa papasa baada ya lile Neno kufanyika Mwili nalo ndio Yesu Kristo mwenyewe (Yohana 1:14).

Kumbe Neno hili halikuanzia kipindi cha Bwana Yesu lakini lilikuwepo kabla hata ya kuwanyika Mwili ambao ni Yesu Kristo. Hivyo neno hili lilichukua maumbile mengi kabla ya kudhihirika katika wakati uliokusudiwa na mbingu!.

Na tumeshaona Neno lenyewe katika maandiko ndio UZIMA s(Yohana 1:1).

Neno hili lilikuwepo Mwanzo kabisa mwa safari ya Mwanadamu, likawa linashuka kuzungumza na Adamu kumpa uzima lilikuwapo pale bustanini Edeni. Ili kuwapa uzima lakini baada ya kukaidi wakafukuzwa waka mbali nalo wakaanza kulitafuta tena wakazuiliwa kuwa nalo karibu.

Baadae tena tunaona linachukua sura ya SAFINA ili kuwaokoa wanadamu na tunaona linafanikiwa kumuokoa Nuhu pamoja na familia yake yaani watu saba tu.

Na baada ya muda linachukua sura ya Mnyama yaani KINDOO(Mwanakondoo) utaona Ibrahimu alipokuwa akienda kumtoa sadaka Isaka kama Mungu alivyomuagiza na Ibrahimu akatii tunaona anakwenda lakini mwisho anataka kumchinja Isaka Mungu akamwambia asifanye hivyo atazame yuko Mwanakondo ndio amtoe badala ya Isaka.

Unaona mambo haya yalifanyika kwa mafumbo na kwa SIRI sana kiasi kwambailikuwa ngumu kwa mwanadamu kuelewa.

Na mwisho kabisa linakuja kutimiza kusudi kuu linachukua sura/umbile la Mwili  wa Mwanadamu lakini linaanzia kwa Melkizedeki lilichukua sura kama kuhani lakini mkuu lakini kwa ajili ya upatanisho lakini lilikuwa halijadhihirika bado.

Waebrania 7:1”Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;

2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;

3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwana Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele……………….Waebrania

7:15 “Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki;[anazungumziwa YESU KRISTO]

16 asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo;

17 maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki”.

Neno hili lilionekana kama Mwamba kule jangwani kuwavusha wana wa Israeli

(1Wakorintho 10:4 “wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo”.)

Katika sehemu zingine linaonekana kama hekalu, nyoka wa Shaba kule jangwani nk

Yohana 3:14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyohivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;
15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye”.)

Na ndio maana mitume walikuwa na ujasiri baada ya kuyaelewa haya mambo

1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;


2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);”

Sasa tukirudi hapo katika kichwa habari hapo juu Huyu Melkizedeki ni nani?  Tayari Sasa tumeshakwisha kujua kuwa ni Mungu mwenyewe katika Mwili alipojidhihirisha kutimiza jambo fulani kabla ya wakati ule uliokusuduwa lakini baada ya hapo linakuja kudhihirika katika wakati wake uliokusudiwa na kukamilisha ukombozi wetu. Nalo Neno hilo linafanyika kuwa Mwili yaani YESU KRISTO Mwokozi wetu Haleluya!,

Ubarikiwe sana,
Shalom!, Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *