Fahamu maana ya kiburi cha uzima,

  Maswali ya Biblia

1 Yohana 2:16-17
[16]Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.


[17]Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.

Kiburi cha uzima, kiburi hichi kinapatikana ndani ya mtu pale ambapo wingi wa mali za dunia zimeongezeka juu yake, mtu ambaye yupo mbali na Mungu au hamjui Mungu Maisha yake anakuwa anayaweka kwenye mali, anapojiona ana mali nyingi anajiona amefika(anao uzima) asipokuwa nazo anajiona kama yeye sio kitu,…Na akishapata mali anaanza kuinuka moyo na kuwa na kiburi kinachopelekea kubadilika tabia mbele za Mungu na hata Mbele za watu..

Biblia inasema..

Luka 12:15-21[15]Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.

[16]Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;

[17]akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.

[18]Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.

[19]Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.

[20]Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?

[21]Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa

Mungu.

Swali la kujiuliza..

Na wewe uzima wako umeuweka wapi, ni kwenye nini? Kwenye mali ulizo nazo, mashamba na nyumba unazojenga? Je ni magari na fedha ulizo nazo zinazokufanya umdharau Mungu na uone kama hakuna Mungu duniani,je nini? Ni elimu nzuri na vyeo ulivyonavyo vinakupa kiburi hata kuidharau injili na kuona ni mambo yaliyopitwa na wakati, ikiwa kuna lolote limeumbika ndani yako basi fahamu una kiburi cha uzima, na kiburi hakitokani na Mungu, kwasababu vyote hivyo ni kama maua leo ipo Kesho haipo, usijitumainishe navyo kabisa..

Umejiwekea hazina wapi wewe,ni duniani Au Mbinguni, na utajiri wako ni wakiduniani au Mbinguni,

Bwana Yesu atuwezeshe tusiweke na kiburi hiki cha uzima..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT