fahamu maana ya Yohana 12:24 Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake.

Maswali ya Biblia No Comments

JIBU

Katika mfano huo Yesu alitaka wajifunze kwa nini Mungu alimtukuza namna ile, leo hii tunajua ni kiasi gani Mungu alimtukuza mwokozi wetu Yesu Kristo kwa viwango vya juu. Yeye ndiye mtu maarufu kuliko watu wote duniani hajawahi kutokea kama yeye na hatatokea kamwe, jina lake linatajwa kila sekunde ulimwenguni kote…Mpaka kufikia mataifa makubwa kutaka kuja kumuona Yesu, na wengi walikuja si kwa lengo la miujiza bali kuupata wokovu wa Bwana wetu, mpaka wayunani nao walitaka kumuona Yesu…

Yohana 12:20-21[20]Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu.[21]Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu.

Lakini tunaona Bwana kuliona hilo na kuona mwitikio mkubwa vile wa watu wengi kutoka mataifa mbalimbali… Aliwaambia..

Yohana 12:24 Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi”.

Aliutoa mfano huu ili kuonyesha jinsi Mungu alivyompokea, jinsi alivyotukuzwa kiasi hiki, na sisi wa kizazi hiki ndo tunaelewa jinsi Mungu alivyomtukuza Bwana Wetu Yesu Kristo,,tunafahamu hakuna mtu aliye maarufu duniani kote kama Yesu Kristo, anayetajwa na kuzungumziwa kila dakika na sekunde, na jina lake limekuwa likitajwa kwa kila wakati, ni YESU KRISTO, haleluya haijalishi kutakuwa na watu maarufu au watatokea wangapi lakini yeye Mwamba wetu atabakia kuwa namba moja maana yeye ndiye maarufu duniani kote…

Lakini tunaona siri ya yeye kuwa hivi ni katika huo mfano wa chembe ya ngano , anawambia ngano isipotupwa chini ardhini, ikaoza ikakaa sehemu chafu na mwisho wake ikafa kabisa basi fahamu haiwezi kuleta mazao kwa kuzaa chochote, kwasababu itaendelea kuwa vile vile miaka nenda miaka rudi , na hii ni kanuni inayojulikana hata kwa mbegu nyingine…

Ndiyo yaliyomkuta Bwana Yesu Kristo, alikubali kufa kwa ajili ya ulimwengu..

Isaya 53:3 “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.”),

Ulimwengu haukumpenda kwa kitendo cha yeye kuchukia dhambi , ilifikia hatua akaonekana kama amerukwa na akili, Soma (Marko 3:21)

Maandiko yanasema alikuja kwake wala walio wake hawakumpokea (Yohana 1:11)..ilifika hatua Yohana alikiri kabisa kwa ndugu zake ulimwengu hauwezi kumchukia wao, bali yeye kwasababu anazishuhudia kazi zake ni mbovu…

Hiyo ni kuonyesha jinsi gani Bwana Yesu alivyojikana nafsi, alikubali aoze kwa mambo ya ulimwengu , tazama leo Mungu amemtukuza, amempandisha juu , amemfanya mataifa yote wamsujudie ,usidhani ilikuja juu juu tu, ndo hapo tunaona anawaambia wanafunzi wake..

Yohana 12:24-26
[24]Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.


[25]Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.


[26]Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.

Tujiulize kwa nini leo hii tunasema tumeokoka lakini wokovu wetu upo palepale hatuna badiliko lolote kiroho? Ni kwa sababu hatujakubali kuoza kwa habari ya mambo ya ulimwengu. Tumeokoka lakini bado tunauendea mwenendo wetu wa kale, tunataka kuonekana wa kisasa tuvae tunavyotaka, tuendelee kuketi katika mizaha na kuhudhuria sehemu za starehe hatutaki mafundisho mengi tunapenda mafundisho kidogo yenye kututabiria mafanikio n.k.


Tukiendelea hivi Bwana Yesu anasema hatutakuwa na tofauti na mbegu ambayo haijaanguka katika ardhi na kuoza hatutakuwa na matunda yoyote yale kiroho tutahudhuria ibaada kila wakati na kubaki kama tulivyo hatuna ushuhuda wowote.

Leo hii mtu akiulizwa ni jambo gani Mungu kakutendea tangu ulipookoka atasema hajaona chochote,na hapa hatuongelei kuhusu pesa maana kuna walio na pesa lakini hawajabarikiwa, baraka sio lazima ziambatane na pesa. Hapa tunazungumzia mafanikio ya kiroho, je tangu uokoke umepanda viwango vya kiroho au uko palepale?


Damu ya Yesu imebadilisha nini katika maisha yako, je Roho Mtakatifu yupo ndani yako kukushuhudia kuwa wewe ni mwana wa Mungu? Wokovu wako umeleta mabadiliko kwa wengine? Je umejitenga na dhambi kiasi gani?

Kama hakuna chochote basi ujue mbegu yako haijaoza ndo maana haizai matunda. Amua kutubu leo huku ukijua toba inaambatana na kujikana nafsi yako tanguliza msalaba mbele, ya dunia yote yawe nyuma.

Uwe tayari kuchekwa kuonekana mshamba kwa ajili ya maisha ya wokovu, hapo ndipo tunasema umeoza, mbinguni unaonekana umepoteza nafsi yako unaamua kufa kabisa yanapokuja mambo ya ulimwengu kisha Mungu anaanza kukuchipua anakukuza kutoka hatua moja kwenda nyingne unapanda viwango vingine vya juu, unauishi wokovu katika uhalisia wake.

Kisha utashangaa Mungu anakufikisha sehemu ambayo wewe mwenyewe hukutegemea kufika vyote ulivyopoteza anavirejesha ndipo utakuwa na mafanikio kila sehemu. Hivyo wapendwa tujikane nafsi zetu tumfuate Kristo anatungojea ili sisi pia tuinuliwe kama yeye tutoke hapa tulipo.


Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *