FAHAMU MAANA YA ELOHIM,

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana wetu Yesu Kristo atukuzwe karibu katika kujifunza maneno ya Uzima..

JIBU

Jambo la kwanza kulifahamu na kulikumbuka kila wakati ni kuwa katika lugha yetu ya kiswahili neno ELOHIM, hamna mahali linaonekana likitajwa katika biblia yetu kwasababu halipo katika lugha ya kiswahili.

Neno Elohim ni neno ambalo lipo katika lugha ya Kiebrania likiwa linamaanisha MUNGU… Tukisoma kitabu cha mwazo sura ya kwanza kabisa maandiko yanasema, Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi”.. Hii ni katika lugha yetu ya kiswahili lakini tukitafsiri katika kiebrania inasomeka kama hivi; Hapo mwanzo ELOHIM aliziumba mbingu na nchi.Hivyo unaona tofauti hapo? na neno hili limeonekana katika agano la kale takribani mara 2500 katika biblia ya kiyahudi, lakini katika lugha yetu ya kiswahili limetafsiriwa kama Mungu.

Muda mwingine hili neno ELOHIM limefupishwa kama “EL” ..Na ndio maana sehemu nyingine anajulikana kama EL’Shadai ikiwa inamaanisha kuwa yeye ni “Mungu mwenyezi” kwa lugha yetu ya kiswahili (Mwanzo 17:1, kutoka 6:3 )..Sehemu nyingine anatajwa na kutambulika kama EL ROI, ikimaanishaMungu anayeona”(Mwanzo 16:13)..

Halikadhalika sehemu nyingine anatajwa kama El Elyoni ikiwa na maana kuwa yeye ni “Mungu aliye juu”…majina haya yote utayakuta katika nakala za biblia ya kiebrania tu . Pia mahali pengine tunaona Bwana Yesu akitamka hili jina kama lilivyo, hasa pale alipokuwa msalabani tunaona alisema..EL’OI ELOI lama Sabakthani…maan yake ni Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?..

Tufahamu ya kuwa jina la Elohimu maana yake ni Mungu ikimaanisha kwamba ni Mungu asiyekuwa na mwanzo, wala mwisho, Mungu mwenyezi, muweza wa yote, muumba wa vinavyoonekana na visivyoonekana, n.k. kwa kufupisha ni kuwa jina la Elohimu limebeba tabia zote za Mungu Mwenye enzi Yote..

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *