Fahamu maana ya Ayubu 20:5 shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo,

  Maswali ya Biblia

Karibu tujifunze Maneno ya Mwokozi Wetu Yesu Kristo..

Ayubu 20:4-7[4]Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale, Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi,

[5]Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo, Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu?

[6]Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikilia mawinguni;

[7]Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe; Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?

Biblia inasema hata watu waovu wanazo siku za shangwe lakini sios za siku nyingi ni za muda kitambo tu. Unaweza kumuona mtu ni tapeli na muuaji na bado anaishi vizuri tu ana amani, na mafanikio, mambo yake yanaenda vizur ana afya nzuri n.k. Ukiona hivyo usistaajabu maana neno halijasema watapata shida kila siku, Biblia haijasema hivyo…


Maandiko yanatuambia wanaweza kuwa viwango vya juu kuliko kawaida hata kuifikia mbingu yaani wanaweza kuonekana kama miungu duniani. Lakini mambo hayo yote tunayoyaona kwao hayadumu ni ya muda tu siku wakifa yanaishia hapo hapo.

Biblia inaenda mbele zaidi ikituonyesha kuwa watapotea milele kama ‘Mavi’ yanavyopotea na sote tunajua huwezi kutafuta kinyesi chako ulichojisaidia mwaka jana au mwaka juzi maana huwezi kukitambua kilishaingia chooni kikachangamana na maji machafu na kupotea ndivyo ilivyo hata kwa watu waovu ambao wapo bize kutafuta raha za duniani kuliko kutafuta raha ya milele iliyopo mbinguni kwa Mwokozi Wetu Yesu Kristo..

Zaburi 92:7[7]Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele;

Yesu alisema itamfaa nini mtu akapata vitu vyote vya ulimwengu halafu akapoteza nafsi yake? Tutambue kuwa hatupo hapa duniani kwa ajili ya kula na kunywa au kujenga majumba ya kifahari na kutafuta umaarufu, tupo hapa ili kufanya mapenzi ya Mungu kwanza kisha ndipo tutafute mambo mengine.

Ndugu mpendwa kubali kuokoka na kuishi kulingana na Neno la Kristo yaani biblia takatifu ili usipotee kama waovu bali upate shangwe milele…


Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT