JE SHETANI ANAISHI WAPI? AMEFUNGWA AU YUPO KUZIMU?

  Maswali ya Biblia

Shalom mwana wa Mungu karibu tujifunze maneno ya Mungu…

Baadhi ya watu wanafikiri kuna mahali shetani amefungwa na atakuja kufunguliwa badae na wengine wanaamini anaishi kuzimu au chini ya bahari sehemu ambayo ameweka utawala wake unaofanana na wa hapa duniani..

Jambo moja tunalotakiwa kujua ni kwamba shetani hajafungwa na wala haonekani katika umbo la mwili bali anafanya kazi katika ulimwengu wa roho, kwasababu baada ya kumuasi Mungu alitupwa hapa duniani kisha akaanza kuwadanganya wanadamu na kufanikiwa kuuteka ulimwengu na kuumiliki..

Luka 4:5-7[5]Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.

[6]Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.

[7]Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako..


Umeona hapo, na kitu kingine ni kuwa shetani hana makao rasmi anazunguka zunguka tu duniani, tunaliona hilo kipind akizungumza na Mungu,

embu tusome

Ayubu 1:6-7[6]Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao.

[7]BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.

lakini ukifika wakati wa utawala wa amani wa Yesu wa miaka 1000 hapo ndipo shetani atafungwa na kufunguliwa tena badae muda mfupi ila kwa wakati huu yupo kila mahali akiwapotosha watu katika uovu..

Shetan yupo katika ulimwengu wa roho na mapepo yake wakifanya kazi kila mahali wamegawanyika sehemu tofauti tofauti kama vile angani, wengine katika familia na mataifa mbalimbali, wengine katika huduma fulani au kanisa kazi yao kubwa ni kuuharibu ulimwengu..

Njia ya kumshinda ni kumpa Yesu Kristo Maisha yako na kukesha katika maombi kwa kusoma na kulishika neno la Mungu..

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT