USIKWEPE MATENGENEZO YA AHADI ZA MUNGU KWAKO.

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo alie Bwana na mwokozi wetu. Karibu tuyatafakari maneno ya mwokozi wetu.

Wakristo wengi tunapenda kusikia Mungu akituahidia ahadi mbali mbali katika maisha yetu, na tunatamani tupokee tu bila kutaka kujiandaa ama kukubaliana na matengenezo/gharama za ahadi hiyo.

Kama vile mzazi anavyomuahidia mtoto wake kumfungulia biashara Fulani. Kwa mzazi anaejitambua ni lazima atalazimika kumfundisha ni namna gani ile biashara inatakiwa iendeshwe ili isife kama mzazi hana ujuzi huo atatafuta mtu mwenye ujuzi huo ili amfundishe. Sasa ni lazima mtoto akubali matengenezo yaani kufundishwa asipokubali hivyo na hana ujuzi na biashara ile ni lazima biashara ile itakufa lakini pia wakati mwingine inaweza kumpoteza hata yeye akaishia kuwa ni mtu wa anasa nk.

Au mtu aliemuahidia mtoto wake kumpa gari hawezi akampa hata kama gari lipo na halitumiki kama hajui kuendesha wala hana leseni. Maana kama akimpa na hajui kuendesha atakakapojalibu kuendesha ni lazima atapata ajali na anaweza kuangamia yeye pamoja na gari pia. Hivyo mzazi hawezi mpa gari hilo ikiwa mtoto huyo ni mzembe ama anakataa kufundishwa kuendesha lile gari litendelea kuwepo ila wakati atakapokuwa na uelewa lile gari atapewa.

Sasa kama wanadamu tunafanya hivyo je si zaidi kwa Mungu wetu? Vivyo hivyo Mungu anapotuahidia kutufanyia jambo Fulani katika maisha yetu huenda alishakuahidia jambo Fulani ndugu tambua ni lazima utapita katika kipindi cha matengenezo tu na kadili unavyozidi kuwa mtii na mwaminifu katika kipindi hicho ndio ile ahadi inavyozidi kukaribia kutimilika kwako.yaani unaivuta kwa haraka maana iipo tayari ila inasubilia wewe uwe tayari ili uweze kukipokea.

Hivyo leo tutaangalia baadhi ya mifano kadhaa ambayo Mungu aliwaahidia watu lakini ilibidi kwanza wapiti kwenye matengenezo kabla ya kuifikia ile hadi na tutaona tabia za watu hao zilikuwaje!.

I. WANA WA ISRAELI.
Bwana aliwaahidia wana wa Israeli kuwatoa Misri kwenye utumwa kwenda kwenye nchi imiminikayo maziwa na asali Kaanani. Na walifikiri itakuwa ni kutoka Misri tu na kufika katika nchi hiyo huenda walifikiri hata ni mwendo wa siku kadhaa tu watakuwa wamefika.lakini haikuwa hivyo ilibidi wapitie kwanza kwenye matengenezo. Na bahati mbaya hawakulifahamu hili(na hakuna mtu anaefahamu kuwa anapita kwenye matengenezo ya ahadi ile ataona ni mateso na Mungu yuko mbali nae). Matokeo yake wengi wakaanza kulalamika na kumnung’unikia Mungu. Walitaka kufika tu kwenye nchi ya ahadi ila hawakuwa tayari kuandaliwa.

Kutoka 17:2 – 4 “

[2]Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu Bwana?

[3]Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung’unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu?

[4] Musa akamlilia Bwana, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe.”

Unaona hapo!, watu hawa walianza kunung’unika si kwamba walikuwa hawajui wanakoelekea ni wapi? Walikuwa wanajua kabisa lakini wao hawakutaka matengenezo na wengi wakashindwa kuifikia ile ahadi ambayo walikuwa wameahidiwa.

TUNAJIFUNZA NINI KATIKA HILI?
Tunapoahidiwa ahadi na Mungu wakati unapopitia vipindi vigumu usiwe ni mtu wa kulalamika kuwa mtu wa kushukuru na kusonga mbele maandamu yeye ameahidi atatenda. Manung’uniko yako hayatamfanya Mungu afanye bali yatazidi kuiweka ile ahadi mbali hata kama Mungu amesema na wewe mara 100.
Jaribu la Mungu litakalo kupata ni yeye kukukaria kimya kwa kipindi Fulani aone je? Utaendelea kusonga mbele?, Mungu aliwakalia kimya wana wa Israeli siku tatu tu! Lakini walishindwa kusonga mbele na kuanza kunung’unika.

II. YUSUFU.
Wengi wetu tunajua Mungu alisema na Yusufu kwa ndoto na kumuonesha kuwa siku moja ndugu zake watamuinamia.(Mwanzo 37:7-8).


Mwanzo 37:9 “Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia.”


Lakini ahadi hii haikutimilikia wakati huo huo lakini ilikuja kutimilika akiwa na miaka kama 30 na hapo katikati alipitia matengenezo ya namna mbali mbali moja wapo ni kuwa mkuu wa nyumba ya Potifa na baadae kwenda gerezani karibu miaka miwili na alikaa kwa uaminifu.

NINI TUNAJIFUNZA?
Tunaona yote yaliyompata Yusufu kamwe hakuacha kushikamana na Mungu katika mazuri na katika mabaya Yusufu bado alikuwa pamoja na Mungu na alikuwa ni mwaminifu na baadae anakuja kukiri na kutambua kuwa alipita kule kote Bwana alikuwa akimuandaa. Ndio maana hatuoni hata akiwachukia ndugu zake waliomfanyia vile.

Mwanzo 45:8” Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri.”


Unaona hapo anasema “” Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu…………” kuna watakati Mungu atakupitisha katika njia tofauti na unazozitarajia kabisa. Lakini kuwa mwaminifu wala usianze kuuliza uliza Mungu huku ni wapi mbona napotea!?. Endelea kusonga mbele mtazame Bwana yeye ndio ameahidi wala si mwadamu atafanya kwa majira na wakati wake.

III. MUSA.
Kama tunavyojua mambo yote yaliyompata Musa hata akakimbia Misri na kwenda kufika midiani.

Lakini Musa alipofika kule ndio kilikuwa ni kipindi chake cha matengenezo kwa kipindi cha miaka karibu 40 lakini aliendelea kuwa mwaminifu katika kulichunga kundi la kondo na mwisho wa siku Bwana anamtokea katika kijiti kinachowaka moto na kumpa maagizo yote. (kuwaongoza wana wa Israeli kutoka Misri kwenda kaanani kwa kipindi cha miaka 40 jagwani).

Ipo mifano mingi sana ambayo hatuwezi kuieleza yote ila kupitia hii namini tumejifunz jambo.

Ndugu ni jambo la kutafari sana huenda Mungu kakuahidia kukupa kazi nzuri lakini kila unapopeleka barua ama maombi hupati, kasema na wewe utakuwa ni mtumishi wake mkubwa lakini unaona hiyo dalili hakuna, unaposoma biblia huelewi na ni muoga kuhubiri injili kwa watu,na pengine umehubiri sana watu hawaokoki wanakudhikaki nk

Huenda kasema na wewe mambo mengi lakini huoni yakitimilika zaidi sana watu wanakuona umerukwa na akili ndugu nataka nikutie moyo na ujasiri pia endelea mbele usichoke wala kukata tamaa. Uko kwenye kipindi chako cha matengenezo ongeza nia na juhudi yeye aliesema ni mwaminifu. Usianze kunung’unika wala kukosa uvumilifu,tumaini na utii songa mbele ukijua ipo saa yeye asiebadilika atafanya.

Waebrania 13:8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele”

liamini Neno lake ni yakini. Usitishwe na mazingira ya nje. Shetani hutumia hayo kukukatisha tamaa kama kule jangwani alivyowakatisha tamaa na wakaona kana kwamba Bwana hawezi kufanya jambo. Mungu hatishwi ama kufanya jambo kwa sasabu ya mazingira ila anafanya jambo Muda unapofika haijalishi ni mazingira gani.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *