Kitendo cha kumpa mtu uthamani anaostaili au hadhi ya juu iliyo yake inajulikana kama Heshima, kwasababu Kiuhalisia kila mwanadamu anapenda kushehimwa au kupata heshima, kwa upande wa mtu aliye mpokea Yesu ana sababu nyingi za kujua anaigawanya vipi heshima kulingana na makundi au watu husika, kwasababu kinyume cha kukosa heshima maana yake una kiburi(Mithali 15:33) ukikosa heshima inaweza kukuondolea baraka zako au kibali unapotamani kufanya jambo fulani ili lifanikiwe, na kuitoa heshima isiyompasa mtu inakuwa ni makosa..
Warumi 13:7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima
Tuangalie aina za Heshima unazopaswa kuzijua na kuzitenda
- Heshima kwa Mungu Wetu
1) Heshima kwa Mungu ipo Katika kuliamini pamoja na kuliishi Neno lake kama linavyosema, wala si Katika kulitamka jina lake na huku uko kinyume na maneno yake, anasema hapa Luka 6:46 Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo? 47 Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake
2) Uaminifu Katika kumtolea Mungu sadaka zako na matoleo yako ni heshima mbele za Mungu, Mithali 3:9 Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote
3) Kumfanyia Mungu ibada, Kwasababu anayestahili yote,kusujudiwa, kuabudiwa ,kuinuliwa kupewa sifa na utukufu na utukufu,ni Mungu mwenyewe peke yake wala si mwingine yoyote Mwanadamu au mnyama bali ni Mungu, anayestahili heshima hii kubwa ni Mungu..Ufunuo 4:11 “ Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa”
- Heshima kwa wazazi wetu
1)kuonyesha kutoa msaada kwa wazazi kwa kuwasaidia Katika mahitaji yao ni heshima pia..(Mathayo 15:1-7)
2) Kuwa mtu wa kusikiliza na kuyashika kwa kutii maagizo yao,Mithali 1: 8 Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,
- Heshima kwa viongozi wako wa kiroho
Kusikiliza maelekezo yao,
Waebrania 13:17 Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.
- Heshima kwa Watoto
Kutowaletea makwazo..
Waefeso 6:4 Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana
- Heshima kwa viongozi wa nchi
Kuwa mtendaji wa maagizo yao
Warumi 13:1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu
- Heshima kwa mabwana
Kuwa mtumwa kwa kutenda Katika Uaminifu na adabu (Waefeso 6:5-8)
Hivyo kwa pamoja kila mwanadamu anastahili heshima, awe ni mtu maskini,awe ni tajiri,anafaa au hafai, ni mgonjwa au kilema, amempokea Bwana Yesu au bado,ana elimu ya juu au hana kabisa,jambo kuu ambalo ni agizo la Mungu ni kuwa wanadamu wote wanapaswa waheshimiane…
Shalom..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.