Daawa ni nini kama tunavyosoma Katika Maaandiko?

  Maswali ya Biblia

Daawa ni madai, shitaka, malalamiko, au hukumu inayoweza kutokea pale mshirika mmoja anapomdhulumu au amekufanyia jambo baya.

1Wakorintho 6:1 “Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?


2 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?


3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya”?

Biblia inashauri kwamba wanapokuwa na malalamiko dhidi ya ndugu Wakristo, wanapaswa kuyawasilisha mbele ya kanisa na kuyaamua wao wenyewe, kwani Mungu amewapa jukumu la kuhukumu mambo ya mwili kwa haki. Hivyo basi, hakuna sababu ya kupelekana mahakamani.

Mistari mingine inayoeleza juu ya Neno hili, ni kama ifuatayo:


Ayubu 31:13 “Kama nimeidharau daawa ya mtumishi wangu, au ya kijakazi changu, Waliposhindana nami;


14 Basi Mungu atakapoinuka nitafanya nini? Naye atakapozuru, nitamjibuje?


15 Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni”?

Kumbukumbu 16:19 “Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki”.

Kumbukumbuku 17:8 “Ikiwa limezuka neno lililo zito kukupita wewe, katika maamuzi kati ya damu na damu, na kati ya daawa na daawa, na kati ya pigo na pigo, nayo yashindaniwa katika malango yako; ndipo nawe uondoke, ukwee uende mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako”;
Mengine ni hii: (2Samweli 15, Ayubu 5:8, 23:4,29:16,35:14)

Jiunge na channel hii kwa Mafundisho zaidi,

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Kama ujampokea Kristo(kuokoka) kwa moyo wako amua leo Bwana anakupenda sana.
wasiliana nasi kwa namba hizi: +255693036618 au +255789001312.

LEAVE A COMMENT