Neno kujazi lina maana gani?

  Maswali ya Biblia

“kujazi” katika maandiko linamaana ya “kulipa” linahusu kutoa au kutoa sadaka bila nia ya kuonekana mbele za watu.

Mathayo 6:2 “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.

3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;

4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.

inasisitizwa kwamba wakati mtu anatoa sadaka bila nia ya kuonekana, Mungu atawalipa.

Katika Mathayo 6:6 “Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi…

Mathayo 6:17 “Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;

18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.

inashauriwa kuomba mbele za Mungu na kufunga kunapaswa kufanywe kwa nia ya kumtukuza Mungu sio ili uonekana au kusifiwa/kushindana na watu kwamba ni wa kiroho sana.

Ruthu 2:11 “Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikilia watu usiowajua tangu hapo.

12 Bwana akujazi kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake”.

Tunaona pia hapa Boazi akimbariki Ruthu, kwa wema wake aliomfanyia mkwewe, na kumwambia Bwana akulipe kwa kazi yako njema.

Ujumbe uliotolewa na Bwana juu ya “kujazi” ni kwamba hakuna tendo jema tunalomfanyia Mungu halitarudisha malipo ikiwa tutalifanya ipasavyo. Tukiomba mbele za Mungu kweli, tukafunga kwa ajili yake, tukampa sadaka zetu, na kutenda mema yo yote, tunajua kwamba Bwana atatulipa tu kwa wakati wake, na thawabu yako haitakupita.

Jiunge na channel hii kwa Mafundisho zaidi,

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kama ujampokea Kristo(kuokoka) kwa moyo wako amua leo Bwana anakupenda sana. wasiliana nasi kwa namba hizi: +255693036618 au +255789001312.

LEAVE A COMMENT