DALILI YA KUANGUKA KWA MWAMINI.

Biblia kwa kina No Comments

Bwana Yesu asifiwe ndugu katika Kristo Yesu karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Kama mwamini uliyemuamini Yesu Kristo kweli kweli na kusimama thabiti katika imani kwa muda mrefu na Kristo ziko dalili ambazo ukiziona hizo ndani yako jua kabisa kama usipokuwa makini na kutaka kupiga hatua mbele jua kabisa unakwenda kuanguka tena anguko kubwa sana.

Tutakwenda kutazama kwa kina dalili moja wapo kwa kina ambayo ukiiona hii basi jua kabisa uko hatarini na huna budi kukataa hali kama hiyo mapema ili uwe salama!.

KURUDIA MAMBO YA ZAMANI/ULIYOYAACHA.

Unapomwaamini Yesu Kristo anakupa nguvu ya kushinda mambo mengi mabaya ndani yako sasa unapokaa katika wokovu ukaanza kuona yale mambo ambayo ulikuwa umeshaanza kuyaacha  unaanza kuyarudia basi jua kabisa uko hatarini hebu tusome jambo moja hapa halafu tulitafakari kwa kina..

2 petro 2:22 “Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, MBWA AMEYARUDIA MATAPIKO YAKE MWENYEWE, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.

”Ni kwa namna gani unayarudiaje matapiko yako mwenyewe?“SIKU ZOTE UNAPOANZA KURUDI NYUMA NI LAZIMA UTAANZA KUYARUDIA  MAOVU AMA DHAMBI ULIZOKUWA UNAZIFANA KABLA HUJAMWAMINI YESU KRISTO” wala huwezi kutoka nje na hayo, mzunguko wako utakuwa mle mle tu wala hutafanya jambo ambalo ulikuwa hulifanyi.

Kama ulikuwa unajichua utarudia tena kuanza kujichua, kama ulikuwa unaangalia picha za uchi mitandaoni utaanza tena kuangalia, kama ulikuwa unanyoa viduku utaanza tena kunyoa viduku, kama ulikuwa mvutaji wa sigara, mtumiaji wa pombe, bangi utaanza kuvirudia tena, kama ulikuwa ni mvaaji wa vimini na suruali kwa mwanamke utaanza tena kuvaa, ulikuwa ni muangaliaji wa filamu za kidunia na msikilizaji nyimbo za kidunia utaanza kuzirudia tena,

Kama ulikuwa ni mzizi utaanza tena uzinzi, nk hutatoka nje ya dhanbi ya ulizokuwa unazifanya kamwe.

Lakini haitakuwa kawaida kama ulivyokuwa ukifanya mwanzoni bali itakuwa ni maradufu ya hapo yaani utajikuta unafanya zaidi ya ulivyokuwa unafanya hapo mwanzo  Kama maandiko yanavyosema.

2  Petro 2:20 “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.”

Unaona hapo anasema “…… wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho IMEKUWA MBAYA KULIKO ILE YA KWANZA.”

Ndugu yangu jitafakari na uangalie katika maisha yako ya wokovu ni mambo yapi umeanza kuyarudia na unaanza kuona ni ya kawaida tu na wakati mwanzoni Bwana Yesu alikupa nguvu ya kuyashinda mabaya hayo je umeanza kurudia tena uzinzi,  pombe unakunywa kwa siri siri? Je umeanza kujichua tena? Na kuangalia picha za uchi na kusikiliza miziki na tamthilia za kidunia hali moyo wako ukikudanganya ni sawa tu wala hakuna shida lakini wakati mwingine maaandiko yanakushuhudia na dhamiri yako inakushuhudia huko si sahihi! Ila unajitumainisha.

Ndugu yangu kuwa makini tuko katika nyakati za mwisho hizi kuwa makini na maisha yako unayoishi ya wokovu ukiona umesimama nga’nga’ania wala usiachie kabisa wokovu wako ulinde na kuutunza kuwa na kiasi, jizuie na mambo ya ulimwengu huu ya kitambo tu hebu kuwa makini sana na wokovu wako usihadaiwe na mambo ya ulimwengu huu kuwa makini katika roho angalia usije ukaanguka tena dhambini.

1 Wakorintho 1:12 “Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.”

Ukisoma kwenye tafsiri ya kiingereza inasemaa…

1 Corinthians 10:12”Therefore let anyone who thinks he stands [who feel sure that he has a steadfast mind and is standing firm ] take heed he fall[into sin].”

Unaona hapo anasema! .”……..take heed  he fall[into sin]” maana yake na aangalie asije akaanguka katika dhambi.

Hivyo kuwa makini ukijua kabisa hutatoka nje na dhambi ulizokuwa ukizifanya kabla hujampa Yesu Kristo maisha yako.

Ubarikiwe sana.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *