Elewa maana ya kuota UNAKEMEA MAPEPO

  Ndoto

Shalom karibu katika kujifunza maneno ya Uzima

Hali ya kuota unakemea mapepo au unashindana na nguvu za giza, inakuwa ina maanisha maana tatu kwanza ni unapitia kweli vita vya kiroho, pili Mungu anakuonesha uhalisia wa vita vya Rohoni, tatu ni kuoneshwa uwezo au Hali yako kiroho

Tukisoma..

Waefeso 6:12-13
12″ Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.”

1. VITA VYA KIROHO
Katika vita vya kiroho kuna nyakati adui huanzisha mashambulizi katika ndoto, Ndipo unaona umeota unakabwa na wachawi au majini na unahangaika kitandani kiuhalisia kabisa hiyo ni vita.
au unaota umedhuriwa na nyoka katika kidole na punde unapoamka unahisi maumivu katika kidole, zaidi ya hapo Inaleta kidonda, na mwishowe maumivu mwili mzima. Sasa ndoto aina hizo ambazo unaona uhalisia wake kwa nje, Basi mpendwa hayo ni mashambulizi ya adui, Na unayo mamlaka ya kuyashinda kwa JINA LA YESU KRISTO.

2. MUNGU ANAKUONESHA UHALISIA WA VITA VYA KIROHO
Wakati mwingine sio kwamba unakemea au kushindana na mapepo Bali unaoneshwa uhalisia wa vita vya Rohoni vilivyopo halisi kabisa aidha katika maisha yako muda huo, au vitakuja mbeleni katika maisha yako. Na inakupasa uvishinde katika Jina la Yesu Kristo, na kusimama imara katika Hilo.

3. MUNGU ANAKUONYESHA KIWANGO CHA KIROHO ULICHOPO
Au unachopaswa uwe nacho, Sababu kuna wapendwa waliookoka lakini Wana hofu dhidi ya kukemea mapepo au kufanyia watu Maombezi. Sasa katika ndoto hii Mungu anakuonesha kuwa uwezo wa kufanya hivyo unao, na inakupasa uanze kuombea wengine walio katika vifungo vya Giza.
Unapoona katika ndoto unazidiwa na nguvu za haya mapepo, hiyo inaonesha udhaifu ulionao katika Roho, hivyo inakupasa uanze kuongeza Viwango vyako kwa Maombi, Utakatifu na neno la Mungu ili uwe imara zaidi dhidi ya Maadui.

Hivyo pindi unapoona unakemea au kushindana na wachawi kwa JINA la Yesu kristo ni wakati dhahiri kabisa wa kuwa imara na Bwana dhidi ya adui yako  Shetani. Ili umpige kwa thabiti rohoni kuwa hakika Umeokoka.

Endapo kama hujaokoka unayo Leo nafasi ya kufanya hivo, mkaribishe Yesu maishani mwako, ukitambua kwamba humshindi shetani Kwa nguvu zako ila kwa yeye Bwana Yesu Kristo.

Maranatha

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT