Je easter ni sikukuu ya kibiblia?

Maswali ya Biblia No Comments

JIBU..

Sikukuu ya kiyahudi ijulikanayo kama Pasaka ilianza rasmi kipindi cha wana wa Israeli wanatoka nchi ya misri, ndipo Mungu akawapa agizo la kupaka damu ya mwanakondoo  Katika miimo ya na nguzo za milango yao ili yule malaika atakayepita kuua wazaliwa wa kwanza asiwadhuru wazaliwa wao..

Hata malaika yule alipopopita na kuiona ile damu ya mwanakondoo alipita juu asiwadhuru, hakuingia Katika hiyo nyumba…

Tendo la malaika huyu kupita juu ndilo lijulikanalo kama Pasaka, au Kwa lugha ya kingereza inajulikana kama Passover…

Tujiulize easter ni nini na ipo kimaandiko?

Jibu ni kwamba hatuoni neno easter likitajwa popote kwenye maandiko ukiangalia kama neno pasaka tunavoliona likitajwa, neno easter halipatikani kabisa..

Hivyo kama halipo, limetoka wapi sasa Katika Imani ya Ukristo

Easter ni mungu wa kipagani mwenye asili ya mwanamke, walimwamini kuwa ana uwezo wa kuleta uzao kama mungu baali alivyokuwa, mungu huyu wa kike alifanyiwa ibada na watu waliojulikana kama watu wa sexons ambao kwa kipindi hiki ni watu wa ujerumani, na walimwita jina hilo easter kwa vipindi vya mawio ya jua, linapochomoza jua upande wake waliamini ni upande uliojaa neema unaoweza kumfaa mungu mke, kwa upande wa mashariki ni “East” kwa kingereza, hivyo kwa kumpa heshima ndio wakamwita easter, ikimaanisha “wa mashariki”

Na kipindi kile cha sikukuu za kiyahudi mungu mke alikuwa anatolewa sadaka za Kafara , tarehe hizi zilienda sambamba/ pamoja, wakati wana wa Mungu,wa Israel wanasheherekea Pasaka na ndicho hicho kipindi watu hawa wa sexons wanakwenda kutoa sadaka za Kafara kwa mungu wao mke(easter)

Si jambo la kushangaa kwasababu shetani kazi yake ni kutafuta kuchanganya Ukristo na upagani, aliweza kuinua makundi ya watu na kuoainisha sikukuu ya Pasaka na siku ya easter ambayo ni siku ya mungu wao,

Sasa ili kumbukumbu la mungu wao lisiondoke wala kufa kabisa kabisa ndipo wakaiweka siku ya Jumapili ambayo ni siku ya kufufuka kwa Bwana wakaiita, ‘Jumapili ya easter’

Je na Wakristo wanaruhusa kuiadhimisha easter kama ni siku ya kufufuka kwa Bwana Yesu

Sikukuu ya kufufuka kwa Bwana Yesu itabaki kuwa pale pale ni vema na kupendeza kuiadhimisha, kwasababu ni siku tuliopata ushindi na uzima wa milele, ni siku ya furaha na shangwe kwetu,siku ya faraja na matumaini,baba wetu wa imani, (mitume) na watakatifu kipindi cha zamani walijificha na kujifungia ndani Kwa hofu ya wayahudi, ilipotimia siku wakamwona Bwana amefufuka walijawa na furaha isiyo na kifani…

Luka 24:34-41

[34]wakisema, Bwana amefufuka kweli kweli, naye amemtokea Simoni.

[35]Nao waliwapa habari ya mambo yale ya njiani, na jinsi alivyotambulikana nao katika kuumega mkate.

[36]Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.

[37]Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho.[38]Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu?

[39]Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.

[40]Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake.

[41]Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa?

Watakatifu wa Mungu tuna kila sababu ya kuiadhimisha siku hii ya Pasaka ya kufufuka kwa Bwana Yesu, (Jumapili ya Pasaka) ingawaje itajulikana kwa majina mengi tofauti tofauti,hata wangeitambulisha kama siku ya kumwabudu shetani, hatuangalia ni majina gani waliyotoa kwenye siku, tunaiangalia siku yenyewe,

Kwasababu hata siku za kuzaliwa kwetu zina majina na maana mbaya lakini hiyo haimfanyi mtu kuacha kuiadhimisha kwa kuwa zimefanana na tarehe zenye mambo mabovu..

Hivyo kwa WaKristo wanasheherekea siku ya kufufuka kwa Bwana Yesu ijulikanayo kama JUMAPILI YA PASAKA, na Sio Easter, na kusheherekea kwetu hatusheherekei kipagani..

Tunapoiadhimisha siku ya kufufuka kwa Bwana Yesu halafu tunakesha bar kulewa fahamu kabisa hapo unaisheherekea easter, tunapoisheherekea siku ya kufufuka kwa Bwana Yesu huku tunakwenda disco, makumbi ya anasa, jua hapo unamsheherekea mungu mke,easter na sio ufufuo wa Bwana

Kwa desturi yao waliokuwa wanamsheherekea huyo mungu mke , desturi yao ilikuwa ni kulewa na kucheza wanapokwenda kutoa sadaka zao..

Bali wana wa Mungu tunaiadhimisha siku ya kufufuka kwa Bwana Yesu kwa kumfanyia ibada, kwa kumtafakari Mungu kwa Wokovu mkuu aliotupa, na kutafakari toka tumepata wokovu ni hatua gani tumepiga Katika kumjua, ni kukaa na kuangalia ni wapi umeenda tofauti ili upate kutengeneza mambo mengi ya rohoni,kwa kumuimbia Mungu na kumsifu kwa Matendo makuu aliyotufanyia..

Shalom, Maran atha…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> 

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *