Fahamu Nini maana ya ndoto UNAENDESHA GARI AU CHOMBO CHA MOTO 

  Ndoto

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu katika maneno ya Uzima.

Asilimia 95 ya ndoto tunazoota mara kwa mara au Kila siku zinatokana na sisi wenyewe au mawazo yetu wenyewe mfano shughuli za Kila siku( Daily activities ), Mawazo au mazingira yanayotuzunguka.

Hivyo ndoto za Namna hii hazibebi Ujumbe wowote wa kiroho, yakupasa uzipuuzie La sivyo utachanganyikiwa kwa kudhani Kila unachokiota kina maana.

Hapana shaka kwamba unapoota ndoto Ambayo haihusishi mazingira yanayokuzunguka, au mawazo ya Kila siku, Basi huyo ni Mungu akisema nawe jambo Fulani kupitia ndoto.

Kuota Unaendesha gari au umewapakia watu kwenye gari ni ishara ya kwamba unaongoza maisha yako na ya watu pia, katika kuwafikisha mahali Fulani.

Endapo upo ndani ya Yesu unalitimiza kusudi lake, zidisha mwendo katika safari hiyo, maana hakika Lengo utalifikia kama tu hutopunguza mwendo kama Yehu, katika jukumu la kwenda kumwua mfalme muasi Yoramu na Mamaye Yezebeli. Uzembe huu ulipelekea Israeli kushiriki uchawi na ibada za sanamu Ambayo ni machukizo makubwa kwa Mungu

Soma.

2 Wafalme 9:20

“Yule mlinzi akatoa habari, akasema, Amewafikilia wala harudi tena; na mwendo huu ni kama mwendo wa Yehu mwana wa Nimshi; MAANA ANALIENDESHA GARI KWA KASI

Angalia, hii inatufundisha ukiwa na kusudi la Mungu mkononi mwako, imekupasa kulitimiza pasipo na mitazamo ya watu.

Kwa kuongezea…..

Ni vyema kuzingatia ni gari la aina gani unatumia kuliendesha kusudi la Mungu?

Mfano mfalme Daudi alikuwa akilisafirisha sanduku la agano la Mungu kutoka Abinadabu mpaka Yerusalem.

Tunaona Daudi anafanya kosa kubwa hapa, Anatumia Ng’ombe kuliendesha kusudi la Mungu, badala ya watu au makuhani ambao Mungu aliwataka walibebe Kila wakati, hii inapelekea kifo Cha mtu

Soma…

1 Mambo ya Nyakati 13:7-10

7″ Wakalipandisha sanduku la Mungu juu ya gari jipya kutoka nyumba ya Abinadabu; na Uza na Ahio WAKALINDESHA LILE GARI.

8 Wakacheza Daudi na Israeli wote, mbele za Mungu, kwa nguvu zao zote; na kwa nyimbo na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa matoazi, na kwa tarumbeta.

9 Hata walipofika penye uga wa Nakoni, Uza akaunyosha mkono wake alishike sanduku; kwa maana wale ng’ombe walikunguwaa.

10 Ndipo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Uza, naye akampiga, kwa sababu alilinyoshea sanduku mkono wake, hata akafa pale pale mbele za Mungu.”

Unaona? Kumbe imetupasa kufanya kusudi la Mungu na wale tunaowaongoza kwa kuzingatia kigezo Cha kimaandiko.

Ndipo inakuja sababu ndio Maana Kila mtu anaota anaendesha vyombo mbalimbali baiskeli, pikipiki n.k ili Hali inahusisha kuendesha tu, kitu Cha msingi ni kutimiza kusudi la Mungu kwa Ukamilifu.

Ishara ya ndoto hizi ni mbaya sana kwa mtu ambaye hajaokoka, Maana huenda anajiongoza au kuongoza wengine katika dhambi

Turejee..

 2Mambo ya Nyakati 21:12-15

12 “Likamjia andiko kutoka kwa Eliya nabii, kusema, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako, asema hivi, Kwa sababu hukuziendea njia za Yehoshafati baba yako, wala njia za Asa mfalme wa Yuda;

13 lakini umeiendea njia ya wafalme wa Israeli, _UKAWAENDESHA KATIKA UASHERATI_ Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; tena umewaua ndugu zako wa nyumba ya baba yako, waliokuwa wema kuliko wewe;

14 tazama, Bwana atawapiga pigo kubwa watu wako, na watoto wako, na wake zako, na mali yako yote;

15 nawe utakuwa na ugonjwa mkuu kwa maradhi ya matumbo, yatakapotokea matumbo yako kwa sababu ya ugonjwa huo siku kwa siku.”

Mfalme huyu Yehoram  yaani mwabudu sanamu, mchawi na mwuuaji n.k Sasa katika Maovu yake haya anaendesha Wana wa Israel kutenda dhambi ya hatari ya uasherati wa kiroho . Hivyo Mungu alimpiga kwa mapigo Yale.

Mpendwa, Bwana anakupenda sana ndio Maana anakuonya utubu na umgeukie, Ili gari la Maisha yako ukaliendeshe katika njia sahihi ya kusudi la Mungu na si lile la Shetani.

Amen

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT