NUHU ALIJENGA SAFINA KWA MIAKA MINGAPI?

  Maswali ya Biblia

Jina la Bwana wetu yesu Kristo litukuzwe.

Karibu mwana wa Mungu tujifunze neno la Mungu kwakuwa neno la Mungu ni Mungu mwenyewe.

Nuhu alijenga safina kwa miaka mingapi?

Kabla hatujajua hili swali hebu tujue maana ya neno safina.

Safina ni nini?

Ni chombo Cha majini kilichotumika katika ukombozi. Mfano kwa Nuhu hiki chombo kilitumika kumkomboa Nuhu, wanyama, ndege n.k.

Katika biblia haijaweka wazi kuwa safina ilijengwa kwa muda Gani japo baadhi ya watu wanasema ilijengwa kwa miaka kufuatia kitabu Cha

mwanzo 6:3, inasema BWANA akasema, roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwakuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.

Lakini Haina Maelezo yaliyojitosheleza kuainisha hili japo kwa upande mwingine biblia inasema Nuhu aliwazaa watoto wake akiwa na miaka 500 kama ilivyoandikwa katika kitabu Cha

mwanzo 3:32 inayosema

“Nuhu alikuwa na miaka mia Tano, Nuhu akawazaa shemu, na Hamu, na yafethi.

Kwa upande wetu tunahitaji kufahamu zaidi ni hili Dunia ya kwanza iliangamizwa kwa gharika ya maji kutokana na maovu yaliyotendwa na wanadamu. Na pia katika hii Dunia yetu ya pili itagharikishwa kwa moto kutokana na maovu wanayoyatenda wanadamu.

Na Chanzo cha gharika hilo la kwanza ni dhambi kama wivu, uzinzi, rushwa, chuki, fitina, ulevi, ushoga, ulawiti, usagaji, lugha za matusi, tamaa mbaya na nyingine nyingi.

Hivyo inatupasa kumcha BWANA kwa kuuchukia uovu na kutenda yaliyo mema ili hili gharika la pili ambayo ni ya moto isitukute yatupasa kumpokea BWANA awe mwokozi wa maisha yetu na tuache dhambi unyakuo unakaribia.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT