KUWA MKRISTO KWELI KWELI.

Biblia kwa kina No Comments

KUWA MKRISTO KWELI KWELI.

Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe.

Kuna kuwa mkristo, lakini pia kuna kuwa mkristo kweli kweli. Bwana Yesu alipomuona Nathanieli alimtambua kuwa ni mwisraeli kweli kweli, maana yake kulikuwa na waisraeli wengi, lakini katikati ya hao waisraeli kuna waisraeli kweli kweli ambao ndio hao wakina Nathanieli.

Yohana 1:45 “Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.

[46]Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone.

[47]Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, TAZAMA, MWISRAELI KWELI KWELI, HAMNA HILA NDANI YAKE.

[48]Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona.

Na halikadhalika hata katika uisraeli wa rohoni (ukristo), kuna wakristo wa kawaida (wakristo jina) na wakristo kweli kweli.

Mkristo kweli kweli ni yupi?

Mkristo kweli kweli ni yule aliyejikana nafsi yake na kuchukua msalaba wake na kumfuata Yesu. Kama yeye mwenyewe alivyo sema katika..

Marko 8:34 Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.

Lakini wakristo wengine wa kawaida tu, hawajajikana nafsi zao wala kuchukua misalaba yao na kumfuata Yesu. Bado wanaupenda ulimwengu, hawataki kuacha udunia, ukiwahubiria waache uasherati wa kidunia, wachome nguo zao za aibu na waondoe vyombo vyote vya uzuri… kwa maana ni machukizo kwa Mungu. Wanasema tunaenda na wakati, wanaogopa kuitwa washamba, wanaogopa kutengwa na ndugu au marafiki, kupotea kazi, kupoteza heshima zao n.k, hawa ndio waisraeli tu lakini sio waisraeli kweli kweli.

Je! upo kundi gani? We ni mwisraeli tu au mwisraeli kweli kweli.

Kama bado unafanana na watu wa dunia hii, kimuonekano au kimazungumzo, mwanamke unavaa suruali, vimini, nguo za kubana, unasuka, unapaka kucha rangi, unavaa hereni, vikuku, unajipodoa, we ni kijana unacheza magemu, unafuatilia mipira, movies, miziki, unabeti, unanyoa denge, unavaa modo, unaishi na girlfriend au boyfriend na hampo kwenye mpango wa kuingia kwenye ndoa takatifu , mnachati chati tu kizinzi, basi tambua we ni mkristo jina tu!!

Ni heri leo ukaamua kumgeukia BWANA YESU na kuwa mkristo kweli kweli.

Kumbuka ukifa katika hiyo hali ya uvugu uvugu (ukristo jina), unashuka moja kwa moja KUZIMU. Ni heri uchague kuwa mpagani kweli kweli… huwenda mapigo yako yakawa tofauti kidogo huko uendako.!!

Amua leo kujikana nafsi na kuubeba msalaba wako, wacha dunia ikuone umechanganyikiwa lakini wewe unajua unayafanya mapenzi ya Baba yako aliye mbinguni..

Bwana Yesu alisema..

Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? ( Marko 8:36 ).

Itakufaidia nini uonekane wa kisasa halafu huendi mbinguni??

Kumbuka pia tunaishi ukingoni mwa nyakati na Yesu Kristo yupo karibu sana kurudi kuchukua watakatifu wake.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *