Elewa tafsiri  ya Mithali 16:30 Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka; 

Maswali ya Biblia No Comments

Mithali 16:30[30]Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka; Aikazaye midomo yake hutokeza mabaya.

Andiko hilo halina maana kuwa kufumba macho kunapelekea mtu kuwaza yaliyopotoka, sivyo, kwasababu ikiwa itamaanisha hivyo, vipo vinavyofanyika , kwa mfano tunapoomba kwa kufumba macho basi ingekuwa tunafanya makosa..

Hekima inapokuwa ndani ya mtu inampelekea kuona aibu hata kufumba macho yake wakati jambo la kikatili au uovu wowote unaoendelea,kama walivyofanya  watoto wa Nuhu..(Mwanzo 9:23)

Pia inapozungumzia mtu aikazaye(aifumbaye)midomo,hana maana mtu asiyezungumza zungumza, Mwisho wake huzungumza yasiyofaa..

Mithali 21:23
[23]Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake,
Atajilinda nafsi yake na taabu.

Lakini je? Vifungu hivyo vilimaanisha Nini?

Biblia inaposema hivyo,afumbaye macho yake ni kutazama mabaya inamaanisha, afumbaye macho yake asitazame kweli ya Neno la Mungu, unapoonywa na Neno la Mungu,likikufundisha Katika njia mbaya unazoziendea na ukakaidi ujue apo umefumba macho yako, unapoambiwa uvae mavazi ya kujisitiri lakini ukatia moyo mgumu usisikie ujue umekusudia kuendelea kwenye njia zako mbaya..

Ndio mana Bwana Yesu alisema hivi…

Mathayo 13:15
[15]Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito,
Na kwa masikio yao hawasikii vema,
Na macho yao wameyafumba;
Wasije wakaona kwa macho yao,
Wakasikia kwa masikio yao,
Wakaelewa kwa mioyo yao,
Wakaongoka, nikawaponya.

Lakini pia anaposema aikazaye midomo yake hutokeza mabaya,anamanisha anayeizuia midomo kuzungumza Maneno ya Uzima, yenye kujenga,yenye kuleta busara na mshikamano basi Mwisho wake atakuwa akinena Maneno mabaya yaliyojaa uovu..

Luka 6:45
[45]Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.

Hatuna budi na sisi kujichunguza kila siku,je macho yetu yanatazama nini, midomo yetu inazungumza Maneno gani, fahamu kuwa kwa nguvu zako mwenyewe hautaweza kushinda ikiwa Kristo ajatawala ndani yako, njia ni nyepesi ni kwa kumwamini tu na kuyaweka maisha yako kwake akusamehe dhambi,ili upate nguvu ya kushinda dhambi..

Yesu Kristo ndiye njia, kweli,na Uzima…

Haleluya..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *