Tafsiri ya Mithali 11:17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake.

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Mtu mwenye rehema ni mtu mwenye huruma, asiyeshikilia chuki,wivu,hasira, visasi,  ni mtu mwenye kusamehe watu wengine hata kama amekosewa na alistahili kutoa huku juu ya mtu alie mkosea yeye anachilia kabisa.

Maandiko yanasema mtu wa namna hii anaitendea mema nafsi yake. Na Biblia inasema pia kwa kipimo kile kile tupimacho ndicho hicho hicho tutakachopimiwa tena na zaidi ya hapo.

Marko 4:24 Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.

Mtu kama huyu anajitengenezea mazingira mazuri na kuzidi kujiweka katika hari nzuri katika roho yake Lakin pia kupata faida katika huu ulimwengu na ule ujao wa milele.

Kama maandiko yanavyosema.

Mathayo 5:7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.

Hivyo mwenye kusamehe, anayofaida kubwa sana katika ufalme wa Mbinguni.

Kinyume chake mtu asiekuwa na rehema yaani mtu mkali asiesamehe,anaekaa na visasi,chuki,wivu hasira, vinyongo na uchungu,  mtu wa namna hii moja anajitaabisha mwenyewe pili hata katika ufalme wa Mungu.

Kama Bwana alivyosema katika Neno lake tusiposamehe kama sisi tulivyosamehewa na Baba yetu vivyo hivyo nasi hatutasamehewa.

Maana pia na wewe wapo watu wengi unaowakosea kwa kujua ama kwa kutokujua hivyo Mungu hataki tuwe watu wa kukaa na visasi, kulipiza baya kwa baya bali tunapotenda mema/kuwa watu wa Rehema basi tutazidi kuupendeza moyo wa Mungu sana.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *