Nini maana ya neno hedaya kwenye biblia? (zaburi 68:29)

Maswali ya Biblia No Comments

Hedaya ni neno linalomaanisha Zawadi ,na ili kuonyesha pongezi au shukrani kwa wema uliofanywa basi inapelekea kutoa zawadi..

Neno hili limetajwa katika maandiko..

Zaburi 68:28-29
[28]Ee Mungu, uziamuru nguvu zako;
Ee Mungu, uwe hodari uliyetufanyia makuu.


[29]Kwa ajili ya hekalu lako Yerusalemu
Wafalme watakuletea hedaya.

Zaburi 76:11
[11]Wekeni nadhiri, mkaziondoe
Kwa BWANA, Mungu wenu.
Wote wanaomzunguka wamletee hedaya,
Yeye astahiliye kuogopwa.

Isaya 18:7

[7]Wakati huo BWANA wa majeshi ataletewa hedaya na watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao; Mpaka mahali pa jina la BWANA wa majeshi, mlima Say

uni.

Wanadamu wote tunajukumu la kumpelekea Mungu wetu hedaya..

Na tunampelekea kwa njia mbili:

Njia ya kwanza,Ni kwa kumwimbia Mungu sifa za vinywa vyetu, kwa shukrani na Matendo makuu aliyotutendea Mungu Wetu,tuna sababu za kumpa zawadi hizo..

Njia ya pili, Ni kwa kumtolea sadaka, unapoonyesha moyo wa kujali kwa Mungu, kumtolea fedha, mali zako unaonyesha moyo wa shukrani na wakujali kwa kutazama ni mangapi Mungu amekutendea hivyo unapeleka zawadi zako za kushukuru kwa sadaka zako…

Shalom…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

  • Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *