Nini maana ya Mafuta mabichi, Zaburi 92:10

Maswali ya Biblia No Comments

JIBU..Tusome

Zaburi 92:10
[10]Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati,
Nimepakwa mafuta mabichi.

Biblia inapozungumzia mafuta mabichi haina maana kuwa ni Mafuta ambayo hayajapitishwa katika moto , hapana,bali ni mafuta yaliyo Katika upya ambayo hayana muda mrefu, kipindi cha agalo la kale na hata sasa walitumia mafuta ya mizeituni Katika Chakula na Matumizi ya ibada, yalitumika kama kiungo cha mboga tofauti na jamii zetu, mmea wa alizeti ndio utumikao kuleta Mafuta kwa ajili ya matumizi mbalimbali..

Ndo mana chakula kilichopikwa kwa mafuta ya mzeituni yaliyo mabichi “yaani mapya”  kilikuwa kina ladha nzuri, hata ile mana jangwani ilifananishwa na mafuta mabichi, (soma Hesabu 8:11). Na Katika Mambo ya ibada, Mafuta ya mzeituni yalitumika kumtawaza Mfalme kama ishara ya kwenda kuchukua madaraka hayo..

1 Samweli 9:15-16
[15]Basi BWANA alikuwa amemfunulia Samweli, siku moja kabla Sauli hajamwendea, akisema,


[16]Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia.

Soma pia1Wafalme 16:12, 1Wafalme 1:34, na 1Wafalme 19:15-16

Njia iliyotumika kwa makuhani ni kwa kupakwa mafuta,kama ishara ya kuchaguliwa na Mungu ili kutumika..

Zaburi 133:2
[2]Ni kama mafuta mazuri kichwani,
Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni,
Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.

Jambo hili lilikuwa la kiheshima kutiwa Mafuta mapya, kwasababu kawaida ya Mafuta haya hudumu miaka miwili tu na baada ya Hapo huaribika yasiweze tena kutumika kwenye shughuli za kiibada au Matumizi ya vyakula.. Mafuta mabichi yalikuwa na utukufu wake..

MAFUTA MABICHI NA YA KALE YANAWAKILISHA NINI ROHONI?

Kiuhalisia Mafuta yanamwakilisha ROHO MTAKATIFU, hivyo mafuta yaliyokaa,ya zamani yanawakilisha utendaji kazi wa Roho Mtakatifu kipindi cha Agano la kale,na Mafuta mapya ni utendaji wa ROHO MTAKATIFU Katika agano jipya.. kwasababu tunahitaji sana Mafuta mabichi Katika utumishi tunaoufanya kwa kuwa yanatufaa sana..

Mafuta mapya yanatufanya kila siku tuenende Katika utakatifu Ili tufikie ukamilifu katika kuyatenda mapenzi ya Mungu kuliko yale ya zamani..

Mathayo 5:27-34
[27]Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;


[28]lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.


[29]Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.


[30]Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.


[31]Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;


[32]lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.


[33]Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;


[34]lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;

Maran atha

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *