Elewa tafsiri ya Mithali 19:11 busara ya mtu huiahirisha hasira yake

Maswali ya Biblia No Comments

Mithali 19:11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa

Kabla ya kuendelea mbele tutazame kwanza Nini maana ya busara
Busara ni kitendo cha mtu kuwa na uwezo wa kaughahiri hasira yake wakati anapoudhiwa mtu na huwa mwepesi wa kusamehe makosa.

ukisoma
Kutoka 34:6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;
7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.

Hiyo ilikuwa sifa pekee ambayo Mungu wetu alikuwa nayo, yeye si mwepesi wa hasira bali ni mwingi wa Rehema, pia mwepesi kumsamehe , ikiwa na sisi tunaitwa Wana wa Mungu hatuna budi kuwa kama Mungu, maana neno la Mungu linasema

1 Petro 1
15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.

Tabia ya kubeba watu moyoni walikosea, iondoe mapema, maana kama usipokuwa mtu wa kusamehe hata BABA yako wa mbinguni hawezi kusamehe ukisoma katika (Marko 11:26) kumbe tusipo samehe na Mungu hatatusamehe ila tunaposamehe wanatuudhi ndipo na Mungu anatusamehe na sisi, yaani hata iwe umeumizwa kiasi gani, usitake kulipa kisasi bali fanyika kuwa mtu mwenye busara siku zote za maisha yako, maana kwa kufanya utaupendeza moyo wa Mungu

Usikasirike haraka pale unapokosewa , embu kabla ya kufanya chochote kaa tafakari kwanza, jiulize je mimi sijawahi kukosea mtu yeyote, ukipata mda wa kutafakari hata maisha yako uwezi ukawa mtu wa visasi, maana hata wewe ulikosea na ukasamehewa…… Angali hata Upendo wa Mungu katika maisha yako hakutazama makosa yako uliyotenda, Bali alikusamehe hivyo hivyo na uovu wako mwingi Sasa kwanini wewe ushindwe kusamehe.
Anza leo upya hiyo tabia ya malipizi iondoe maishani mwako na rohoni mwako na usiishie kuomba My Mungu akusaidie bali jitahidi pia kutenda

Na mambo haya huwezi kuyaweza kwa nguvu zako wenyewe, bila kuwa na Roho Mtakatifu utatesekana sana, utapokea nguvu hii Kwa Mwamini Yesu Kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yako , kisha utabatizwa hapo ndipo utapokea nguvu ya Roho Mtakatifu ambayo itakusaidia kushinda jambo hili

Mungu akubariki sana

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *