NINI MAANA YA NENO ZABURI

  Maswali ya Biblia

Maana halisi ya neno zaburi ni “Nyimbo takatifu” hivyo Katika biblia zaburi ni kitabu cha nyimbo takatifu na zimekuwa takatifu kwasababu lengo lake ni kumfanya mtu amrudie Muumba wake, ni njia moja wapo ya kumwimbia Mungu na kumsifu, ijapokuwa zaburi pia ulikuwa ni unabii wa Mambo yanayokuja mbeleni..

Nyimbo hizo zilitumika pia katika kipindi cha Agano la kale,Wayahudi walizitumia kumwimbia Mungu Katika masinagogi yao, zaidi sana hata wakati wasasa zimekuwa zikitumika Katika utungaji mzuri wa nyimbo nzuri za Kumsifu Mungu…

Na kwa sehemu kubwa kitabu hiki kimeandikwa na Mfalme Daudi ijapokuwa wapo wachache walioshiriki kuandika pia, sehemu kubwa ameandika Daudi,na kumwimbia Mungu alianza kumwimbia akiwa mdogo,biblia imeweka wazi…

Wapo wengine waliweza kuandika nyimbo Katika biblia ingawaje hazikuwekwa kwenye kitabu hiki cha zaburi,Musa pia alishiriki kuandika mfumo huo,zinapatikana kwenye Kumbukumbu la Torati 32..

Jambo la muhimu ni kuwa zaburi hizi zilizoandikwa na Daudi, zimeweza kutukuzwa na Mungu mwenyewe mpka leo, kwasababu zimejaa utukufu,sifa, Upendo kwa Mungu wetu,kumtukuza yeye..

Tuyaangalie maneno haya..

Zaburi 145:1-9
[1]Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza,
Nitalihimidi jina lako milele na milele.


[2]Kila siku nitakuhimidi,
Nitalisifu jina lako milele na milele.


[3]BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana,
Wala ukuu wake hautambulikani.


[4]Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako,
Kitayatangaza matendo yako makuu.


[5]Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako,
Na matendo yako yote ya ajabu.


[6]Watu watayataja matendo yako ya kutisha,
Nami nitausimulia ukuu wako.


[7]Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu.
Wataiimba haki yako.


[8]BWANA ana fadhili, ni mwingi wa huruma,
Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,


[9]BWANA ni mwema kwa watu wote,
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.

Hatuna budi na sisi kumwimbia Mungu kwa sifa na vinanda,kwa shangwe na vigelegele kwa Matendo makuu aliyotutendea Mungu Mkuu

Zaburi 147:1
[1]Haleluya.
Msifuni Bwana;
Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu,
Maana kwapendeza, kusifu ni kuzuri.

Zaburi 149:1
[1]Haleluya.
Mwimbieni BWANA wimbo mpya,
Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT