Nini maana ya haki huinua taifa (Mithali 14:34)

Maswali ya Biblia No Comments

Haki kibiblia ni tofauti na haki kama inavyojulikana na watu wengi, maana haki kisheria inatafsirika kama kile mtu anachostahili kuwa nacho au kile anachoruhusiwa kufanya, au kile anachostahili kupokea kutoka kwa wengine kwa mujibu wa sheria’.

Na maana nyingine haki inafahamika kama watu kutenda matendo mema ni kupata haki .

Lakini kibiblia haki ni tofauti na hayo yote , katika biblia haki inamtafsiri MTU ANAYEMCHA MUNGU ndiye mwenye haki, yaani mtu yeyote anayemcha Mungu huyo Moja Kwa moja anakuwa na haki, na asiye mcha Mungu mbele za Mungu si mwenye

Kwahiyo sasa hata kama mtu afanye matendo mema kiasi gani katika jamii yake, ikiwa kama hamchi Mungu, Mungu hamwesabu kama ana haki…

Na hapo biblia iliposema kuwa haki huinua taifa haikutafsiri haki ya watu kutenda matendo mema, Kwa sababu wapo watu wanaotenda matendo mema ili wajipatie sifa katika jamii yao na wengine wanafanya ili kulitimiza sheria ya nchi au Imani zao za kidini na si kwa ajili ya Mungu yaani hawafanyi kwa Upendo ila kinafiki tu , sasa hayo yote Mungu hausiki nayo,. hapa Mungu anachotazama ni watu kumcha yeye wawepo katika taifa, maana hao wenye haki ndiyo wanafanya taifa linyanyuke, tofauti na hapo wasio haki wakiwa wengi nchi huwa inakuwa katika mstari mwekundu wa kuangamizwa tu.

Jambo hili tunajifunza katika habari ya Ibrahimu wakati pale Mungu alipotaka kuiangamiza sodoma na gomora

tusome

Mwanzo 18:22 “Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana.

23 Ibrahimu akakaribia, akasema, JE! UTAHARIBU MWENYE HAKI PAMOJA NA MWOVU?

24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, WALA HUTAUACHA MJI KWA AJILI YA HAO HAMSINI WENYE HAKI WALIOMO?

25 Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?

26 BWANA AKASEMA, NIKIONA KATIKA SODOMA WENYE HAKI HAMSINI MJINI, NITAPAACHA MAHALI POTE KWA AJILI YAO.

27 Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.

28 Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano.

29 Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini.

30 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini.

31 Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini.

32 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.

33 Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake”.

Jambo lililopelekea sodoma na gomora kuangamizwa kumbe ilikuwa kwa sababu ya kukosekana mwenye haki hata kumi ndani ya mji, na ni dhahiri kabisa mji huo ulikuwa Umejaa waovu wengi, ndicho kitu ambacho kilipelekea sodoma na gomora kuwashwa moto wa kiberiti

Kumbe basi hata sasa unavyoona Amani ipo ndani ya taifa, si kwa sababu wapo watu wengi wanaotenda matendo mema, bali ni kwa sababu ya wacha Mungu wapo ndani ya taifa, ikiwa hawatapatikana ni wazi kabisa Amani ya taifa itapotea na taifa litayumba na si hivyo tu bali kuangamia kabisa , na jambo hili si kimwili hata kiroho linatukumbusha kuhusu “dhiki kuu”

2Wathesalonike 2:6  “Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.

7  Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; LAKINI YUKO AZUIAYE SASA, HATA ATAKAPOONDOLEWA.

8  Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”

Kulingana na andiko hilo, linatujulisha kuwa Ile dhiki kuu itakayokuja, itakuja baada ya kanisa yaani wacha Mungu kuondolewa Kwa sababu Sasa hivi haijatokea kwa sababu yupo azuiaye. yaani Roho Mtakatifu, Hadi kanisa litakapo nyakuliwa, ” ikiwa utataka kupata mafundisho yahusuyo dhiki kuu na unyakuo” utatuma ujumbe kwenye namba hizo hapo chini.

Je wewe ni mmoja wa wenye haki mbele za Mungu, je una mcha Mungu, umeshika maagizo yake, na haki inapatikana Kwa Yesu pekee hakuna njia nyingine inayoleta haki tofauti na Bwana wetu Yesu Kristo, ikiwa kama hutamwamini na kufanya awe Bwana na mwokozi wa maisha yako hutoweza kuwa mwenye haki mbele za Mungu

Wagalatia 2:16 “hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki”.

Mwamini Leo Yesu Kristo ili upate haki ya kuwa Mwana wa Mungu, ili pia uliinue taifa lako.

shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *