Fahamu maana ya Mithali 31:6, Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea.

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Tunaposoma Biblia ndani yake kuna agano la Kale na Agano Jipya,  Sasa katika agano la Kale mambo mengi yalikuwa yakifanyika mwilini yaani walikuwa wanalitimiliza katika mwili.

Mithali 31:6 “Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.

7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake”.

Hivyo mambo mengi aliyokuwa akiyapata mtu yalikuwa yanatatulika kwa jinsi ya mwili japo kusudi la Mungu halikuwa hivyo!, ila kutokana na mazingira na nyakati ikabidi iwe hivyo.

Na ndio maana waliruhusiwa hata kuoa mke zaidi ya mmoja ili kutatua matatizo ama migogoro ya ndoa, na pia waliruhusiwa hata kutoa talaka. Lakini Mungu hakukusudia iwe hivyo.

Ila kutokana na sababu mbali mbali akaruhusu iwe hivyo kwa kitambo tu!.

Mathayo 19:7 “Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?

8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi”.

Lakini pamoja na kufanya hivyo haikuwezekana kutatua migogoro katika ukamilifu wote,wala haikuweza kutatua kiu ya uzinzi, na ndio maan utaona Daudi alikuwa na wake wengi na masuria wengi tu lakini hao wote hawakumtosha yaani kiu ya Uzinzi haikuweza kutatulika ndio maana akahamia hata kwa wake za watu mfano mke wa Jemedali wake Uria(Mama yake na Sulemani hapo mwanzo alikuwa ni mke wa Jemedali wa Daudi jina lake Uria.)

Soma 2Samweli 11 na 12. Kumbe kiu ya uzinzi haikatwi kwa kuwa na wake wengi.

Vivyo hivyo hata katika mambo ya uchungu Moyoni,huzuni,kufiwa nk walikuwa na desturi ya watu walipatwa na matatizo hayo wanawapa kileo yaani Pombe (Divai). Lakini yote hiyo haiwezi kuondoa kweli kweli kwani pombe ikishaisha tu matatizo yanarudi pale pale kama ni uchungu unarudi pale pale.

Sasa katika agano jipya Mungu alileta suruhisho la Mambo yote baada ya Kristo kufa na kukufuka na kupaa mbinguni na Roho Mtakatifu akaja na yeye ndio suruhisho la mambo yote ambayo hayakuweza kutatulika kabisa.

Neno linatwambia…

Yohana 7:37 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.

38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.

39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa”

Hivyo pindi tu Roho Mtakatifu anapoingia ndani ya mtu kwa kumwamini Yesu Kristo, anaanza kufanya kazi ambayo pombe haikuweza kufanya,  anakata kiu ya uzinzi ambayo haikuweza kukatwa kwa kuoa wake wengi, mashaka, na kila tamaa za kila namna yeye anaziondoa kabisa.

Sasa je kutokana na haya yote tunaruhusiwa kunywa Pombe? Jibu ni la!.

Maandiko yametwambia wazi wazi tusilewe kwa mvinyo ambamo Kuna UFISADI, mawazo mabaya nk hivyo ni vyema kutambua wewe upo katika agano lipi na kipi unachotakiwa kufanya. Hivyo ukinywa pombe unatenda dhambi na ukiemdelea hivyo hivyo huna mbingu, maana huko hakuna walevi wenzako.

Waefeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;”

MARANATHA.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *