TAFSIRI YA ZABURI 4:4,Mwe na hofu wala msitende dhambi,

Maswali ya Biblia No Comments

Tusome..

Zaburi 4:4-5
[4]Mwe na hofu wala msitende dhambi,
Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
[5]Toeni dhabihu za haki,
Na kumtumaini BWANA.

Katika andiko hili biblia inasema “Mwe na hofu wala msitende dhambi” hajasema mwe na hofu ila msitende dhambi kwamba hofu ikizidi sana inaweza kuleta madhara, sivyo bali hofu inapaswa kuwepo nyingi..

Na tukiangalia hofu inayozungumziwa hapo sio hofu ya kumwogopa Mwanadamu wala shetani na mapepo yake, bali ni hofu ya kumwogopa Mungu(hofu ya Mungu) ambayo Daudi alisema..

Zaburi 36:1
[1]Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake,
Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.

Na hofu ya Mungu ni ile hali ya mtu kuogopa kwenda kinyume na Neno la Mungu,anakuwa anahofu ya kumkosea Mungu kwa kunena au kutenda, tofauti na mtu ambaye ana hofu ya Mungu ndani yake anakuwa anafanya chochote anachokiona yeye bila kujali anamchukiza Mungu..

Kuna watu Katika Maaandiko ambao hawakuwa na hofu ya Mungu,watu wa nchi ya Gerari Ibrahimu aliyokimbilia..

Mwanzo 20:9-11
[9]Kisha Abimeleki akamwita Ibrahimu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu? Umenitenda matendo yasiyotendeka.


[10]Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili?


[11]Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu.

Wakati tunaoishi sasahivi ni zaidi ya miji ya sodoma na gomora pamoja na gerari, hofu ya Mungu haipo tena ndani ya watu na kupelekea maovu makubwa kutendeka, tukiwa na hofu ya Mungu hatutatenda dhambi..

Jiulize ndugu,hofu ya Mungu ipo ndani yako,wenye hofu ya Mungu wanaogopa kutenda dhambi, wanakaa mbali na ulevi, wanakimbia uasherati, wanakuwa ni watu wa kusamehe wanajitenga na mabaya kwasababu hofu ya Mungu ipo ndani yao..

Bwana atusaidie..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *