Tafsiri ya Mithali 10:22 Baraka ya Bwana hutajirisha, wala hachanganyi huzuni nayo

  Maswali ya Biblia

Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”

Tuelewa kwanza hapo aliposema baraka ya Bwana hutajirisha, aliposema hapo hakumaanisha kuwa kipimo cha kubarikiwa na Bwana, baada ya hapo ni kuwa tajiri tu, hapana maana ukiangalia wapo watu wasio mcha Mungu ambao ni matajiri, na wengine maskini lakini na hao pia ni matajiri Kwa Bwana.
Maana baraka za Bwana hazipimwi kwa mali, bali baraka za Bwana zina kanuni yake, huja kwa mwitikio wa Wokovu.

Lakini tukiendelea mbele anasema” Wala hachanganyi na huzuni nayo”
Hapa anaeleza tofauti iliyopo kati ya baraka za Mungu za yule mwovu, Baraka za Mungu siku zote huwa hazina huzuni, ukilinganisha na zile zinazopatikana penginepo hizo huwa na huzuni na si huzuni bali na majuto makubwa.

Kwasababu gani utajiri huo huwa na majuto?, Mfano unakuta mtu kapata utajiri kwa sababu ya kutapeli, alitapeli mali ambayo haikuwa halali yake, unadhani mtu kama huyo atakuwa na furaha hatoweza, ni sawa tu na mtu aliyepata mali kwa kuua, naye mda wote atakuwa katika hali kuwawaza kukamatwa na kufunga, kiufupi maisha yake yanakuwa katika hali ya mashaka mashaka, furaha hana amani hana, hiyo ni kwasababu ya kile alichokipata si halali..

Si njia hiyo tu na hata wale wanaopata mali kupitia ushirikina kwa Waganga, nao hali yao huwa ni hiyo hiyo watu wa mashaka mashaka, Kwa sababu ya masharti wanayopatiwa, maana unakuta mtu kapewa sharti la kutokulala kitandani awe ana lala chini, au aweke joka ndani ya nyumba yake, au atenge chumba ambacho hapaswi mtu kuingia na ikitokea mtu ameingia anakufa pale pale, mambo hayo ni dhahiri kabisa kuwa yatamkosesha amani hawezi kuwa na furaha atakuwa mtu wa hofu na huzuni hata kama ajitahidi kufurahi lakini atakakapokumbuka kuwa hapaswi kulala kitandani hapo hapo huzuni inamuingia Sasa hayo ni mateso.

Lakini utajiri upatikanao kwa BABA YETU WA MBINGUNI hakuna vitu kama hivyo, Mungu hawezi kukubariki kisha akupe huzuni, mateso, huzuni. nk… kamwe hafanyi hivyo , badala yake Mungu akikubariki siku zote utakuwa na Amani na furaha,
Jambo la kuzingatia baraka za Mungu zinakuja pale tunapoyatenda mapenzi yake sawa sawa na

Kumbukumbu la Torati 28
1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.
3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.

Hakuna baraka nje ya mwokovu, kama utashindwa kujua kanuni ya kupokea kutoka Kwa Mungu ndipo hapo utaona kuwa unalaana na kumbe ni kwa sababu ya kutokujua kanuni kuu. maaana kama ukishindwa kutenda maagizo mwisho wake ni laana

Kumbukumbu la Torati 28
15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.

Unataka Amani na furaha, Mwamini Yesu Kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yako, ili uweze kuishi maisha ya kumpendeza Mungu na kuzipokea baraka za Bwana..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT