Je! kweli Fedha ni Jawabu la Mambo yote?

  Maswali ya Biblia

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Moja ya mistari inayonukuliwa vibaya katika Biblia moja wapo ni huu hasa kwa watu wa Mungu, maana imefika mahali Fedha/mafanikio yanahubiliwa zaidi kuliko Yesu Kristo Mwokozi wetu.

Mhubiri 10:19 “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; NA FEDHA HULETA JAWABU LA MAMBO YOTE”.

Sasa je!, kulingana na andiko hili ni kweli Fedha ni Jawabu la Mambo yote? Jibu ni LA!, Fedha sio jawabu la Mambo yote kwa nini?.

Kama Fedha ni Jawabu la Mambo yote ingeweza kununua Amani, je!, inawezekana Fedha kununua Amani? Jibu ni LA!,

kama Fedha ni Jawabu la Mambo yote ingeliweza kununua uzima wa milele, kusingelikuwa na ulazima wa Bwana wetu Yesu Kristo kufa pale msalabani tena kwa Mateso makali, jibu ni la Fedha haiwezi,  ila damu ya Yesu Kristo pekee ndio inayoweza na ilishamaliza inanena mema juu yetu. Haleluya!.

1 Petro 1:18 “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu

19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo”.

Maandiko yanatuambiwa tumekombolewa kwa damu ya Yesu na sio kwa Fedha na dhahabu,

Pia bado Fedha haiwezi kuzuia kifo pale wakati wa mtu kuondoka Duniani unapofika, lakini watu wenye Fedha wanakufa na Fedha wanaziacha haziwezi kuleta uhai wao tena!.

Ukianza kusoma utaona anaanza kutaja mambo ya Sherehe  “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko…” Karamu kwa jina jingine ni sherehe, Sasa anaendelea kusema “….. na divai huyafurahisha maisha….” Mwisho anamalizia kwa kusema ” NA FEDHA HULETA JAWABU LA MAMBO YOTE.”

Sasa ni nini hasa mstari huu ulikuwa unalenga?, hebu turudi tuutafakari kwa kina tutapata jibu!, maana hakuna lililo sitirika maana Roho Mtakatifu yupo kwa ajiri yetu Atukuzwe Bwana Yesu!,

Sasa kwa mnyumbuliko huu tayari jibu la swali hili tumeshalipata.

Ikiwa na maana kwamba hayo mambo yote yaliyotajwa hapo juu yaani Karamu/Sherehe, divai, ili viweze kukamilika Fedha inahitajika.

Mambo ya kidunia kama ulevi,uzinzi, kumbi za starehe hivi vyote vinahitaji fedha na ndio maana watu waliozamia huku kwa kupigwa na upofu na ibilisi wanatafuta Fedha ili wayafanye Mambo hayo maana wanajua bila fedha haiwezekani wakafanikiwa kuyapata.

Lakini sisi wana wa Mungu Fedha sio jawabu la Mambo yote maana tunaweza kuishi bila Fedha maana Yesu ndani yetu, hivyo sisi hatutegemei Fedha ili tuishi, ila damu ya Mwokozi tu Yesu Kristo.

Na maandiko yanasema wana wa Mungu tusiwe ni watu wa kupenda fedha maana si asili ya mtu aliezaliwa mara ya pili yaani na Mungu kuwa mtu wa kupenda fedha, bali yeye hulidhika na alivyonavyo na kumshukuru Mungu maana kamwe Mungu hawezi kumpugukia wala kumuacha.

Waebrania 13:5 “Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa”

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT