tafsiri ya Mithali 27:6 jeraha utiwazo na rafiki ni amini.

  Maswali ya Biblia

mithali 27:6
Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana. ”

Ukisoma kwa makini kifungu hicho, rafiki aliye kuwa anazungumziwa hapo si rafiki mnafiki Bali rafiki wa kweli mwenye upendo wa dhati Kwa mwenzake, Sasa hapo aliposema jeraha atiwazo na rafiki ni amini, ni kwamba ikiwa huyo rafiki yako atakwambia jambo ambalo litakuumiza lakini litakiwa ni la kweli tu na hata kama litakuumiza kwa wakati huo lakini baadae litakujenga maana atakwambia jambo si kwa ajili ya kukupoteza bali kukujenga.

Tofauti na rafiki mnafiki yeye hata akuone unapotea bado atazidi kukupa maneno ya kukusifia, kukupongeza na kumbe unapotea, tabia ya mtu kama huyo tunanukuu andiko hilo kuwa “kubusu Kwa adui ni kwingi sana”, anakuonyeshea upendo kwa kukufariji na kumbe anajua kabisa unapotea , anajua jambo unalofanya lina madhara makubwa lakini yeye unakwambia jambo hilo halina shida fanya tu, huko ni kubusu kwingi…
Hiyo ndiyo sifa ya shetani, usipokuwa makini utashangaa unapotea kabisa, maana yeye tabia yake ni kupindisha habari unakuta maandiko yapo wazi kabisa lakini adui anayapindisha anakwambia hayo hayakuandikwa kwa ajili yako bali yalikuwa Kwa ajili ya watu wengine wa kipindi hicho na watu kwa kukosa kujua neno nao wanatekwa wanasema kweli kabisa, au dhambi fulani zinafanyika katikati ya watu na bado wanaambiwa Mungu hatazami mwili wako, kwanza umeshasamehewa unao uzima wa milele kwahiyo kuwa huru, Sasa hayo ndiyo mabusu ya mwovu, usipokuwa makini utangaamia kabisa

Lakini tunaye rafiki mwema yeye hutuonya mahali ambapo hapapo sawa na lengo lake si kutukomoa, au kutuumiza, japo maonyo au maneno yake anapoyatoa yanaumiza lakini mwisho wa siku yanaleta tumaini jema ndani ya maisha ya baadae, ndiyo maana ukisoma. kitabu cha wagalatia 4:16 Paulo anasema

“Je! Nimekuwa adui wenu kwa sababu nawaambia yaliyo kweli? ”

Watu wengi wamekuwa wakielezwa ukweli wanaona kuwa mtu yule ni adui, hampendi, hana upendo, ana roho mbaya, mbaguzi, na kumbe siyo hivyo, lakini yeye anakupenda na ndio maana anakueleza yakupasayo ili usingamie
mafano wa mzazi bora kwa mwanae ni pale anapoona mwanae anataka kuelekea pabaya, lazima humwonya ili asingamie sasa kumweleza kule ukweli si kwamba hampendi anampemda ndiyo maana hataki mwanae apotee, tofauti na mzazi mwingine ambaye anaona upotevu lakini anakuwa hana hata mda naye zaidi anamsifia tu ni wazi kabisa lazima yule mtoto apotee

Ufunuo 3:19
“Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. ”

Bwana anakupenda ndio maana anakukemea ili urudi katika njia ifaayo.

ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT