Tafsiri ya Mhubiri 10:9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo;

  Maswali ya Biblia

Andiko hili linazidi kuonyesha hatari ya kazi za mikono zinazotendwa jinsi zilivyo, ametumia mwenye kuchonga mawe kwasababu wajenzi wa zamani iliwapasa kwenda kwenye miamba ili kuchonga mawe kwa ajili ya ujenzi wa majengo yao, na walikutana na hatari nyingi ikiwemo kuangukiwa na mawe na kuwaharibu viungo pamoja na vifaa vyao vya ujenzi kuwajeruhi,

Hivyo pia mfano wa mtu apasuaye miti kwa Matumizi ya mbao, zipo hatari anakutana nazo kwa kuangukiwa na mti wakati mwingine shoka kumponyoka kumjeruhi yeye au aliye karibu naye..

Kumbukumbu la Torati 19:5
[5]kama aingiapo mtu na mwenziwe mwituni kwenda kukata kuni, akapeleka mkono wake na shoka ili kukata mti, likatoka shoka katika mpini, likampiga yule mwenziwe hata akafa; basi na akimbilie katika miji hii mmojawapo awe hai;

Hii ni kufunua nini rohoni?

Kama Watoto wa Mungu, tufahamu zipo hatari tutakutana nazo kwenye kazi ya Bwana ya kwenda kungo’a mapando ya mwovu, kwasababu si wakati wote tutaenda Katika wepesi wa kuvuna Katika shamba la Bwana,kuna wakati tutakutana na kupigwa,kudhalilishwa,kuonewa hata kuuwawa (Mathayo 10:17-19)

Ndo mana tukiangalia ziara za Mtume Paulo, wakati anapanda Ukristo kule Asia na Ulaya,alikumbwa na hatari nyingi ikiwemo kupigwa na mawe,kuteswa na kutishwa kwa maneno makali,wamishionari mbalimbali kama dr Livingstone waliojitoa kuleta injili Africa kipindi cha zamani walikumbwa na magonjwa pamoja na hatari za wanyama wakali..

Hivyo Katika yote Bwana Yesu ametuahidi mambo makubwa kuliko hatari tunazoziona,hatupaswi kuongopa wala kuwa na hofu Kwa namna yoyote huku tukidhami kazi ya Mungu ni kwenda kujichinja,SIVYO, yapo mafanikio makubwa,furaha tusiowezakudhania…Bwana ajataka kutuficha hatari zake ili kwamba tutakapokutana nazo tusirudi nyuma bali tuendelee mbele kuifanya kazi yake..

Bwana akubariki..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT