Bali wengine wanamhubiri Kristo kwa Fitina Maana yake nini? Wafilipi 1:12-18.

  Biblia kwa kina

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo,

Waraka huu kwa Wafilipi Mtume Paulo aliuandika akiwa kizuizini(Gerezani) sasa wakati akiwa kizuizini Kuna watu waliinuka nao wakawa wanahubiri injili lakini kuna waliohubiri kwa nia njema wengine kwa nia ya kumkomoa Mtume Paulo .

Sasa ili kuelewa hili jambo vizurii tusome kuanzia juu kwa makini zaidi.

[12]Lakini, ndugu zangu, nataka mjue ya kuwa mambo yote  yametokea zaidi kwa kuieneza Injili;

[13]hata vifungo vyangu vimekuwa dhahiri katika Kristo, miongoni mwa askari, na kwa wengine wote pia.

[14]Na wengi wa hao ndugu walio katika Bwana, hali wakapata kuthibitika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kunena neno la Mungu pasipo hofu.

[15]Wengine wanahubiri habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina; na wengine kwa nia njema.[16]Hawa wanamhubiri kwa pendo, wakijua ya kuwa nimewekwa ili niitetee Injili;

[17]bali wengine wanamhubiri Kristo kwa fitina, wala si kwa moyo mweupe, wakidhani kuongeza dhiki za kufungwa kwangu.

[18]Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi.

Utaona hapo kundi la kwanza lilikuwa likimhubiri Kristo kwa nia njema likiwa na shauku na kiu ya kuona watu wakimgeukia Kristo pasipo kujali chochote.

Lakini kundi la pili lilikuwa likimhubili Kristo vile vile lakini nia yao kubwa ni kujionyesha kuwa wao pia wanaweza kuhubili zaidi ya Paulo. Hivyo katika kumhubiri Kristo wakati mwingi walikuwa wakimnenea Mabaya Mtume Paulo.

Lakini yote na yote baada ya Paulo kupata Habari hizo akiwa Gerezani ilikuwa ni tofauti jinsi alivyopokea yale mambo yanayoendelea huko nje na badala ya Paulo kukasirika matokeo yake anafurahia kwa kuona hata wale wanaomnenea mabaya wanamhubili Kristo.

Hivyo kwake ilikuwa ilikuwa ni furaha kwake kuona injili bado inahubiliwa!.

Tunajifunza nini  katika jambo hili?.

Tunaona kumbe Injili inayohubiliwa na mtu yoyote ile iwe kwa nia njema ama ya kujipatia Fedha inaweza kuleta matokeo makubwa ya wokovu na watu wakaokoka wakamgeukia Kristo. Na pia kuhubili,kutoa pepo nk mambo haya hayamfanyi mtu kwenda Mbinguni.  Tunaliona hilo katika kile kitabu cha….

Mathayo 7:21-23

[21]Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

[22]Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

[23]Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Vivyo hivyo na sisi tujitathimini je? Tunamhubili Kristo kwa njia ipii? Je kwa Mashindano, kutaka kushindana na mhubili mwingine, nabii fulani, Mtume fulani ama tunamhubili Kristo kwa nia njema? Tukiwa na nia na shauku ya kuona watu wanamgeukia Kristo?

Ubarikiwe sana!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT