Elewa Yakobo 5:9Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango..

  Maswali ya Biblia

Yakobo 5:9[9]Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.

Maandiko hayatupi nafasi ya sisi kuwa watu wa kunung’unika Kwa namna yoyote ile,hata kwa kuonewa, kudhulumiwa au kuaibishwa kwa namna yoyote,hatupaswi kuwa watu wa manung’uniko, kwasababu kuwa mtu wa hivyo kunakufanya kutokuwa na roho ya uvumilivu ndani yako na kumfanya Mungu ashindwe kuwa mvumilivu juu yetu..

Lakini hayo tukimwachia Mungu kwasababu yeye ndiye mwamuzi wetu,ambaye yupo malangoni.. Ikimaanisha YESU KRISTO yupo Karibu na sisi sana,yupo na sisi tunapoonewa,tunapopigwa na kudhulumiwa yeye yupo atatulipa tu kwasababu yupo malangoni mwetu.. Atatulipa kwa wakati huu au siku ile ya mwisho ya hukumu,atatenda kwa haki, wakati mwingine anataka uogope kwasababu ukinung’unika hayupo mbali kusikia..

Wafilipi 4:5[5]Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu.

Tukilifahamu hilo hatuna budi kukaa mbali na manung’uniko yoyote, kwasababu Kristo yupo Karibu nasi kutusika, tusiwe wepesi ya kunena, bali tujifunze kuwa wavumilivu katika mambo yote. Ili Mungu atuachilie neema yake..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT