Nini maana ya tutoapo unabii tutoe kwa kadiri ya imani?(Warumi 12:6)

Maswali ya Biblia No Comments

Warumi 12:5-8
[5]Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.


[6]Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;


[7]ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;


[8]mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.

Kulingana na andiko hilo linatuonyesha jinsi kila  mtu alivyopewa kiwango cha Kipimo cha Neema, na kipimo hicho kinaitwa imani kama tulivyosoma hapo, kumaanisha kuwa kama ni unabii basi kuna kuwa na utofauti wa viwango vya unabii, wengine wanaweza kupewa kujua siri za mioyo ya watu, wengine wakajua majira na nyakati, kuna kupewa taarifa za wazi za watu hapo hapo na wengine hata kwa njia ya mafumbo…vyote kwa pamoja vinajulikana Kama vipimo vya Imani..

Kwa namna hiyo ikiwa mtu atatokea na kulazimisha aone jambo fulani ili aonekane yeye ni mwonaji, mtu huyo tayari kashavuka viwango vya Imani alichopimiwa na Mungu.. Kwaiyo mwisho wa siku atatoa taarifa za uongo ambazo ajapewa na Mungu,atatoa maono ajayaelewa hata na baada ya kuomba asielewe pia lakini kwa kuwa hakutaka kuwashirikisha wenye hekima na maarifa au upambanuzi badala yake atatumia akili zake kufasiri na mwisho wake unakuwa ni upotoshaji na siyo kujenga..

Na karama nyingine zote,ikiwa huna hicho kitu ndani yako usikilazimishe kwa nguvu zako,hauna karama ya Ualimu(kufundisha) basi usionyeshe wewe ni mjuaji na unajua sana kufundisha mwisho wake utawadumaza na kuwapotosha watu kwa udhaifu wa fundisho lako..

2 Wakorintho 10:12-14
[12]Kwa kuwa hatuthubutu kujihesabu pamoja na baadhi yao wanaojisifu wenyewe, wala kujilinganisha nao; bali wao wenyewe wakijipima nafsi zao na nafsi zao, na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili.


[13]Lakini sisi hatutajisifu zaidi ya kadiri yetu; bali kwa kadiri ya kipimo tulichopimiwa na Mungu, yaani, kadiri ya kufika hata kwenu.


[14]Maana hatujitanui nafsi zetu kupita kadiri yetu, kana kwamba hatuwafikii ninyi; kwa sababu tulitangulia kufika mpaka kwenu katika injili ya Kristo;

Kaa hapo hapo ulipowekwa na Bwana,ikiwa Neema ya Yesu itaongezeka ndani yako basi itathibitika tu,usiongeze wala kujiongezea chochote,kuna hatari kubwa sana..

Waefeso 4:7[7]Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *