Fahamu maana ya neno mintarafu (zaburi 17:4)

Maswali ya Biblia No Comments

Maana ya Neno mintarafu,lina maanisha “Kuhusiana na”  mfano mzuri ukitaka kutamka sentesi inayosema, Sielewi chochote kuhusiana na kurudi kwa Yesu Kristo, unaweza kusema” Sielewi chochote mintarafu  kurudi kwa Yesu Kristo, hivyo kiwakilishi cha Mintarafu ni sawa na Neno, Kuhusiana na,

Ndani ya biblia takatifu yenye vitabu 66, Neno hili limeonekana mara mbili, kwenye kitabu cha zaburi..

Zaburi 17:4-5
[4]Mintarafu matendo ya wanadamu;
Kwa neno la midomo yako
Nimejiepusha na njia za wenye jeuri.
[5]Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako,
Hatua zangu hazikuondoshwa.

Zaburi 87: 5 “Naam, mintarafu Sayuni itasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye juu Ataufanya imara.  6 Bwana atahesabu, awaandikapo mataifa, Huyu alizaliwa humo”.

Ikiwa mpaka sasa ujafahamu kuhusiana na kurudi kwa Kristo elewa kabisa upo kwenye hatari kubwa sana, ni heri ukaanza kujibidiisha kutafuta kujua majira na nyakati tunayoishi ili Ile siku usiachwe kwenye unyakuo…

Wakati wowote Yesu Kristo anakuja kuwachukua walio wake,waliotayari kwenda Mbinguni,wewe umejiandaaje..

Shalom..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *