Ielewe Tafsiri ya Mithali 19:21 “Mna hila nyingi moyoni mwa Mtu.”

  Biblia kwa kina

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Kwa kawaida kila moyo wa mwanadamu alieumbwa kwa sura na Mfano wa Mungu. Moyo wake umejaa matamanio ya mambo mbali mbali na katika mambo hayo yapo Mazuri pia yako mabaya. Kuna yanayoonekana kuwa ni mazuri lakini ya siri isiyokuwa dhahiri mbele au machoni pa Mungu.

Mfano tafakari ntu kitu fulani kizuri huenda ikawa gari nzuri,nyumba nzuri, Fedha nyingi lakini nyuma yake katika kupata vitu hivyo nia yake ni kuwakomoa watu fulani au kuwafunga mdomo na kuwatambia.

Hivyo mambo kama haya yakiwemo ndani ya mioyo ya watoto wa Mungu kweli kweli kamwe hayawezi kusimama.

Maandiko yanaweka wazi kabisa katika kitabu cha Mtume Yakobo.

Yakobo 4:2  “Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!

3  Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”

Ukisoma  anamalizia kwa kusema Mathali 19:12 “……lakini Shauri la Bwana litasimama” maana yake Hekima ya Bwana itasimama ichuguzayo mawazo na fikra za Mtu na kufanya maamuzi ya kutoa ama kutokutoa
Hivyo si kila jambo analolitamani mwanadamu ni jema!, la bali Kuna mengine yanaonekana kama ni mazuri lakini kumbe yanaudanganyifu wa kupoteza kabisa kama tunavyosoma..,

Yeremia 17:9 “Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua”?

Hivyo katika Jambo lolote tunalohitaji tuombe kwanza hekima ya Bwana ipite kuchuguza. Na kuruhusu mapenzi yake yeye yatimizwe.

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT