JIbu..
Mithali 27:21 inaposema “Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu; Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake”
Kalibu na tanuru ni maeneo ya moto ambapo madini ya shaba,dhahabu na fedha hupitishwa ili kutenganisha uchafu uliogandamana na madini hayo, na haijawahi kuonekana njia nyingine iliyoweza kufanya madini hayo yang’ae isipokuwa imepitishwa kwenye matanuru hayo makali ya moto yaliyotengenezwa kwa makusudi madini yatoke Katika uzuri wake..
JE SIFA ZAKE NI ZIPI?
Ni mambo yanayomfanya asifiwe Katika hayo, mfano ni muimbaji, lakini moyo wake haujivuni, kutokana na kuimba kwake lakini hana kiburi, ni mtii, mpole ana unyenyekevu wa hali ya juu, pamoja labda na umaarufu alionao lakini viwango vyake vya kiroho ni vile vile, kakamilika kweli..
Mwingine Bwana amempa utajiri lakini ukiyaangalia maisha yake unabaki kushangaa, si mtu wa kujivunia utajiri wake, utajiri wake haufanyi akadharau wengine ,asiwe karibu na Mungu wake wala kudharau wengine, mtu kama huyu ni dhahabu safi kweli kweli…
Tofauti na Mwingine akipata hata elimu kidogo utaona anaanza kubadilika tofauti na mwanzo,anaanza kuchagua makundi ya kuishi nao hata kujichanganya kwenye shughuli za kijamii inakuwa ngumu kwake, na wakati mwingine hutafuta makanisa ya kiroho yanayoendana na hadhi yake..
Kwa mambo kama hayo ndiyo yatakayokueleza tabia yako,na usifiwazo,yawe ni mazuri kwako au mabaya, mwenendo wako ukoje, kujiweka Katika uvaaji mbovu au kujisitiri mwili wako…
Hekima kama hizi zinatupa kutambua mambo ya mtu rohoni,si Katika kuleta mazungumzo wala mwenendo wake,bali Katika vitu vinavyompa sifa, Utakuta ni Mtumishi kweli wa Mungu pindi huduma yake ilipokuwa ndogo alikuwa na unyenyekevu,ni mtu mwombaj,anasaidia watu kulielewa Neno, lakini alipokuja kupanda na Huduma kupata daraja utashangaa ameanza kubadilika,anakuwa ni mtu spesho,huwezi kumuona pasipo mualiko fulani, hata injili yake inaanza kubadilika na kuanza kujinadi mwenyewe,Hapo ndipo panapoeleza tabia halisi ya huyo mhubiri, na sio kule chini alipokuwepo kule alikuwa anaigiza tu.
Kila mmoja anawajibu wa kujichunguza ,Utakaposifiwa, au kupandishwa daraja au viwango Fulani,je nitabaki kuwa yule yule kama Bwana Yesu alivyokuwa, Tuna wajibu wa kuwa waombaji ili Bwana atusaidie Katika mambo yote..
Bwana atusaidie sana..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.