Nini Maana ya Mithali 16:2, ..”Njia zote za mtu ni safi machoni pake”

Biblia kwa kina No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo!.

Kwa kawaida mwanadamu yoyote huwa anaona njia zake zote ni kamilifu na ni sawa machoni pake mwenyewe. Lakini Neno la Mungu linatwambia.

Yeremia 17:9 “Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? ”

Kumbe moyo huwa ni mdanganyifu kuliko vitu vyote!, na hii ndio inampelekea mtu kuziona njia zake kuwa ni safi mbele zake maana moyo umempiga upofu. Hii ni hatari sana.

Kama Neno linavyotwambia katika Mithali…

Mithali 16:2 “Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali Bwana huzipima roho za watu”.

Leo hii ukikutana na wanaokula rushwa na kuhujumu uchumi watakwambia wanachokifanya ni sawa watakwambia…

“Nchi yenyewe hakuna haki rais, mwenyewe anafanya hivi hakuna mwaminifu”

Lakini pia hata watu wanaotoa Mimba nao watakupa sababu ya msingi kabisa “sina uwezo wa kumlea hata nikimzaa au baba yake amesema hayuko tayari kuwa na mtoto kwa sasa, kuliko nimzae nishindwe kumlea bora niitoe mimba siko tayari kuona mtoto wangu Anakosa malezi bora mimi mwenyewe bado sijatulia. Nk”

Pia utakutana na waganga pia watakwambia wanachokifanya kuwa ni sawa kabisa kwani nao wanasaidia Mungu na watakwambia hata sisi tunamuamini Mungu. Ukienda kwa wanaouza pombe nao watakwambia “Mungu amesema tufanye kazi na atabaliki kazi za mikono yetu nk”.

Kahaba nae atakwambia “Nisipofanya hivi nitakula wapi?, familia yangu itakula nini? Mtoto wangu ataishije nk”

Hivyo kila mtu hapo unaona anaona anachokifanya kuwa ni sahihi machoni pake na sio hizo tu bali zote!,

Sasa Mwisho Neno linatwambia “… lakini Bwana huzipima roho za watu..” ikiwa na maana Mungu anazichunguza nia zetu(anazijua nia zetu) yeye hashawishwi na sababu, au kile anachokiona ni sawa yeye ajua nia Zetu.

Anajua nia zilizondani yetu na anafahamu mwisho wa kile kitu ni nini? Ni uzima ama mauti?.

Utaona hata Mafarisayo, waandishi,Makuhani, Masadukayo,wasamaria walikuwa wanajiona kuwa ni watu wenye haki(waliojitenga na dhambi). Yaani watakatifu kuliko wengine.  Lakini kwa nini Bwana Yesu aliwaita ni wanafiki?, ni kwa sababu wao walikuwa ni hodari kuyafuata mapokeo kuliko Sheria ya Mungu, na Sheria ya Mungu walikuwa wanaitimiza ilikusudi wao waonekane na watu,wasifiwe  kuwa wanafunga,wananawa mikono mpaka kwemye viwiko nk. Walikuwa wanajifanya tu kumuita Yesu kuwa ni Rabi(Mwalimu) ilihali ndani wamejaa wivu,hasira,nk Soma (Mathayo 23:1-39).

Hivyo Mungu anapokuita uokoke ama uache jambo fulani usimpe sababu. Kama wale watu walioalikwa kwenda Arusini na wasiende kwa kutoa sababu zao, na mwisho ikawa ni hasara kwao Mungu anapokuita utoke huko tii maana yeye anajua hichokitu unachokitolea sababu anajua mwisho kitakuangamiza nae hapendi uangamie.

Luka 14:16 “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi,

17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.

18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.

19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe.

20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.

21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.

22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi.

23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.

24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamuyangu”.

Hivyo tufahamu kabisa, Mungu hashawishwi na sababu elfu tulizonazo, bali anajua Mwisho wake ni nini.!

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *