MUNGU ANASUBIRI UCHUKUE HATUA.

  Biblia kwa kina

Shalom! Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo!.

Mambo mengi yanashindwa kutoka ndani yetu(kuyaacha) kwa watoto wa Mungu wengi kwa sababu bado hawataki/kuamua(kuchukua hatua). Tabia zilizoko ndani yako wakati mwingine unatamani ziondoke lakini haziondoki, ndio kwanza zinazidi kuongezeka(kuota mizizi) zaidi. yote hiyo ni kwasababu hutaki kuchukua hatua kushughulika na hayo mambo maana Roho Mtakatifu yuko kutusaidia pale tunaposhindwa.

Bahati mbaya unajaribu mara moja au mara tano umeona imeshindikana ndio umeamua kukata tamaa kabisa na kuona hilo jambo haliwezekani lakini kumbe linawezekana.(sio kila mtu ameshindwa sema wewe umeshindwa)

Neno linatwambia

Mithali 24:16” Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.”

Unaona hapo! Anasema “mwenye haki HUANGUKA mara saba” hasemi “mwenye haki HUANGUSHWA mara saba”

Mpaka anaanguka maana yake alikuwa anachukua hatua mfano ya  yakupanda mlima anaanguka anarudia tena na tena mwisho anaweza,

Kuanguka kunakozungumziwa hapo sio kufanya dhambi ama sio kuanguka katika dhambi kama uzinzi, wizi nk LA! Bali katika kujalibu kule anaona kama anashindwa ila anakuwa sio mtu wa kukata tamaa.

Leo hii utamkuta Mkristo anasumbuliwa na uzinzi na Uasherati, kujichua, anazini/kujichua halafu anasema “Mungu nisaidie niache dhambi hii sitaki na leo ndio Mwisho” lakini huyu huyu mtu bado anaendelea kuchati na mzinzi mwenzake, bado anaangalia picha za huyo anaezini nae hataki kuchukua hatua ya kuanza kukata mawasiliano nae, hataki kufuta namba zake au kubadilisha laini kabisa.   Halafu unalia unaomba Mungu akusaidie kuacha uzinzi ndugu unajidanganya mwenyewe hutaweza kamwe kama hutakuchukua hatua,

Unasumbuliwa na michezo ya kubeti ushabiki wa mipira, pombe na dhamiri yako kabisa inakushudia si sawa unabaki kusema “Mungu nisaidie kuacha pombe, utukanaji, kubeti, kushabikia mipira nataka nikutumikie wewe tu nk”  unajidanganya na kusema naamini siku moja Mungu atanisaidia(asante Baba maana umenisikia kwa kutia huruma, Mungu hakusikii kwa sababu ya huruma unayoonesha mbele zake bali kwa hatua unayochukua kujikwamua kutoka hapo), kumbe hujui kashakusaidia ila hutaki kuchukua hatua.

na unatoa na machozi kabisa halafu hutaki kuachana na hao marafiki zako watukanaji, kutaki kufuta magroup ya mipira kwenye simu yako, hutaki kuacha kwenda ukumbini unaposikia mechi unawahi siti za mbele kabisa lakini kanisani huwezi kukaa siti za mbele,

Nataka nikwambie huo utabaki kuwa ni wimbo pendwa kwako wa milele wa “Mungu nisaidie Mungu nisaidie sitaki kuwa hivi” ndugu hutaweza kamwe kama usipoamua kuchukua hatua leo. Unaouwezo huo ndani yako umepewa na Kristo.

Mathayo 5:29 “Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.

30  Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum

Unaona hapo! Anasema “…jicho lako likikusosesha ling’oe ulitupe mbali nawe…” hasemi uliache ama uendelee kuwa nalo bali anasema ling’oe ulitupe mbali maana yake uchukue hatua wewe mwenyewe ya kufanya hivyo. sio Yesu/Roho Mtakatifu ama mchungaji ama nabii, shemasi katika hilo eneo ni wewe mwenyewe.

Lakini anaendelea kusema “Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe;” kama tunavyofahamu mkono kazi yake kubwa hasa ni kushika vitu sasa anasema “uukate uutupe mbali nawe” hizo kampani za watu zinazokukosesha acahana nazo ondoka kabisa bila kuangalia nyuma kusalimisha roho yako.

Huyo binti, huyo kaka haijalishi ni mzuri kiasi gani lakini unaaendelea kumshikilia matokeo yake mnazini na kushikana shikana kijinga ndugu nataka nikwambie utaangamia chukua hatua leo itauma lakini itaisha Yesu atakuwezesha kushinda maana yeye mwenyewe anasema.

Yohana 16:33 “ Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.”

Yeye alieushinda ulimwengu anakaa ndani yetu kwanini ushindwe?, unashindwa na wakina Ayubu, Daudi, Musa nk wao hawakuwa na Roho Mtakatifu lakini wewe unaye tena anakutamani kiasi cha kuona wivu kama maandiko yanavyosema.

Yakobo 4:5 ”Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu HUTUTAMANI KIASI CHA KUONA WIVU?”

Usiseme iko siku vitaondoka nitakuwa sawa SAHAU, wewe ndio yafaa uchukue hatua leo utasema nini siku ile unasema “Mungu mimi nilishindwa kucha kitu Fulani” na huku umepewa Roho Mtakatifu.

Nguvu iko ndani yako umepewa acha kujilegeza ndugu umepewa kabisa huoni kama una nguvu kwa sababu ni mvivu wa kuomba, tutaki kusoma Neno wala kushuhudia, bado unautamani ulimwengu na unasema umeokoka.

Ndugu usiwe Mkristo ambae HAJAOKOKA kuwa Mkristo alieokoka leo.

Utapigaje hatua ya pili mbele ikiwa ya kwanza hujapiga?, kazi yako wewe ni kupiga hiyo hatua moja tu ya pili na nyingine yupo atakaekupigisha naye ni ROHO MTAKATIFU

Maran atha

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT