Je Bwana Yesu alioa mke?

  Maswali ya Biblia

JIBU..

Hapana, Bwana Wetu Yesu Kristo hakuwa na mahusiano na mwanamke yeyote na wala hakuingia Katika ndoa (kuoa).. Makusudi yake makubwa ya kuzaliwa na kuja kuishi duniani ni ili ayafanye na kuyakamilisha mapenzi ya baba yake ambayo ni kumkomboa Mwanadamu aliyepotea , na Katika yote hakuwahi kufanya dhambi hata moja wala kuingia kwenye tamaa..

Yohana 8:46 “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?”

Fikra na mitazamo ya watu wengi walifikiri Bwana Yesu alikuwa kwenye mahusiano na Mariamu Magdalene,jambo ambalo si kweli, na fikra kama hizo zimetengenezwa na shetani ili watu wamwone Bwana kama mtu wa kawaida na kuvishusha hadhi vitu vya KiMungu..

Lakini yote si kitu kwasababu yupo Roho Mtakatifu ambaye ndiye anayeishawishi mioyo ya watu,iwe Katika hila na husuda lakini bado KRISTO atabaki kuwa juu na ulimwengu wote utazidi kumwamini na kuokolewa hakuna anayeweza kulipinga hilo…

Wafilipi 1:18 “Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi”.

Injili ya Yesu Kristo itazidi kuenea na watu watazidi kumwamini na kumtukuza, shetani hawezi kufanya chochote..

Utukufu na Heshima vina yeye Mungu Mkuu, haleluya…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT