Je! Ni kweli Bwana Yesu alishika sabato kuninganana luka 4:16?

Maswali ya Biblia, Uncategorized 2 Comments

SWALI: Je! Ni kweli Bwana Yesu alishika sabato kulingana na luka 4:16?

JIBU: Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo apewe sifa daima milele na milele amina. 

Kwanza kabisa tuanze kwa kuuangalia huo mstari wa injili ya Luka kama inavyosomeka

Luka 4:16   Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; NA SIKU YA SABATO AKAINGIA KATIKA SINAGOGI KAMA ILIVYOKUWA DESTURI YAKE, akasimama ili asome. 

Hapo maandiko yanathibitisha kuwa ni kweli ilikuwa ni desturi ya Bwana Yesu siku ya sabato (Jumamosi) kuingia katika sinagogi, sasa swali ni je! Bwana Yesu kwa kuingia kwake hekaluni na kwenye masinagogi alikua anaishika sabato? Jibu ni hapana, Bwana Yesu alikua aingii kwenye sinagogi au hekaluni siku ya sabato tu bali kila siku kutegemeana na mji aliokuwepo

Luka 21:37 Basi, kila mchana alikuwa akifundisha hekaluni, na usiku huenda kulala katika mlima uitwao wa Mizeituni.


Unaona hapo? Maandiko yanasema kuwa KILA MCHANA, ikiwa na maana ni kila siku na si siku fulani hivyo tunaweza kusema kuwa Ilikuwa ni desturi yake kila siku kuingia hekaluni 

Sasa sinagogi palikiwa ni mahali ambapo Wayahudi walikutana kwa masuala yanayohusu ibada na kujifunza maneno ya torati na manabii na haya masinagogi yalikuwa ni mengi katika kila miji, lakini palikuwa na hekalu ambalo hilo lilikua ni moja tu katika Israel yote ambalo hilo hekalu lilipatikana Yerusalemu pekee.

Sasa katika mji wa nazareti hapakuwa na hekalu kwasababu hekalu lipo Yerusalemu pekee na hivyo Bwana alikua akiingia katika masinagogi  na hekaluni. 

Sasa Bwana Yesu alienda kufanya nini hekaluni na kwenye masinagogi kama hakwemda kushika sabato?

Bwana alikua akienda hekaluni na kwenye masinagogi kwa kazi nyingi sana na baadhi ya hizo ni hizi 

1. Kuwaponya wasio jiweza

Bwana alikua akitumia  muda kuwaponya watu wenye udhaifu mbali mbali kwenye masinagogi na hekaluni, kila siku ikiwemo na siku ya sabato pia.

Marko 3:1  Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza; 

2 wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki. 

3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati. 

4 Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza. 

5 Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena. 

2. kufundisha habari za ufalme wa Mbinguni 

Pia Bwana Yesu aliingia katika masinagogi na hekaluni siku ya sabato kufundisha na sio kushika sabato kama mafundisho potofu yanavyodai.

Luka 13:10   Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. 

Yohana 8:2  Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha. 

Bwana Yesu hakuwahi shika sabato na ndio maana watu wa dini wa kipindi hicho walimshuhudia  kuwa haishiki sabato kama tunavyosoma katika

Yohana 9:16 [a] Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato.

Kwahiyo Bwana Yesu alikuwa hashika sabato kulingana na Luka 4:16 Kwani alishuhudiwa na mafarisayo kuwa huiharifu siku hiyo, sasa swali ni je! Bwana alitengua amri zake mwenyewe jibu ni la ( kwamaelezo zaidi acha mawasiliano yako kwenye boksi la maono ili tukufahamishe zaidi) 

Ndugu yangu mpendwa, siku hizi za mwisho na kuna injili njingi sana lakini si za Mungu wetu mwenye nguvu bali za yule ibilisi muovu, ipo injili ya Mungu ambayo inaleta wokovu wa roho zetu na hata maandiko yana thibitisha kuwa kuna INJILI YA MUNGU

1 Wathesalonike 2:9  Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, tukawahubiri hivi INJILI YA MUNGU. 

Umeona hapo hiyo injili ya Mungu? Na hii injili ya Mungu ilihubiriwa na hawa mitume tunaowasoma katika maandiko. Sasa hii injili ya Mungu iliyohubiriwa na mitume inasema katika

Wagalatia 4:9  Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? 

10  Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka.

Tena hii injili ya Mungu iliyohubiriwa na mitume inasema  tena

Wakolosai 2:16   Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; 

Ndugu yangu, injili ya Mungu haijakulazimisha wewe uishike sabato, lakini kama unaadhimisha siku basi iadhimishe kwa Bwana.

Ndugu yangu mpendwa, wewe ukiona kuwa upo kinyume na hiyo injili ya Mungu na unang’ang’ania kushika siku na miezi, basi fahamu  kuwa hiyo sio INJILI YA MUNGU bali ni injili ya ibilisi na lengo lake ni kukupeleka motoni, hivyo badilika leo ukamwabudu Mungu katika Roho na Kweli na kama bado hujabatizwa basi tafuta ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na ni kwa jina la Yesu Kristo 

Bwana akusaidie kuitii injili ya Mungu. Shalom 

2 thoughts on - Je! Ni kweli Bwana Yesu alishika sabato kuninganana luka 4:16?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *