SWALI: Bwana Yesu aliposema heri walio maskini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni wao.(Mathayo 5:3)? Je Biblia inataka tusilijue Neno la Mungu ili tuwe na nafasi nzuri ya kuurithi ufalme wa mbinguni.
JIBU: Andiko hilo halimaanishi tuwe wajinga katika mambo ya ki-Mungu hapana..
Ingekuwa ni hivyo Bwana asingesema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa..
Kukosa kumjua Mungu kunakuweka katika hatari kubwa sana ya kupotea, kwasababu shetani ndicho anachokitaka kwetu.
Lakini maskini wa roho ni mtu wa namna gani?
Kwa kawaida maskini ni mtu ambaye hajatoshelezwa na vile alivyo navyo. Ana njaa ana kiu, ya kupata, tofauti na tajiri anakuwa amesharidhika, nafsi yake imeshiba, hana haja ya kitu..Sawasawa na maneno ya Bwana Yesu katika.
Ufunuo wa Yohana 3:17
[17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
Tofauti na maskini, yeye huwa anahitaji sikuzote..Sasa watu wa namna hii ambao kila siku wanakuwa na haja na Mungu, hawashibi, hawaridhiki na viwango vyao vilevile vya kiroho..hawa ndio maskini wa roho ambao Kristo anawazungumzia.
Ndio wale mitume na wanafunzi wake ambao walikuwa radhi kumfuata kila mahali alipokwenda, ili tu kumsikiliza..Lakini mafarisayo na waaandishi na wakuu wa makuhani, hawakuwa na haja ya kumsikiliza Bwana kwasababu walijiona wanajua torati yote..wanamjua Yehova, wakongwe katika imani.
Hivyo kwa kuridhika kwao hivyo wakaukosa wokovu.
Hivyo Bwana anatakumbusha kuwa kiu yetu kwake kila siku isipungue nguvu, bali tuizidishe, tuwe tayari kuwa kama watoto wachanga kila siku, tusijione tumefika, tusijione tunajua kitu..
Bali tusome Neno, tuombe kwa bidii, tuutafute uso wake kana kwamba ndio tumeokoka leo japokuwa tuna miaka mingi katika wokovu.
Hicho ndicho Bwana anataka kukiona kwetu sote.
Bwana atusaidie sana.
Mada zinginezo:
Biblia ni nini? Je Neno hilo lipo katika biblia yenyewe?.
NANYI KWA SUBIRA YENU MTAZIPONYA NAFSI ZENU