SWALI: je! Majuma sabini aliyoambiwa Daniel kuwa yameamriwa kwa watu wake wamekwisha timia?
JIBU: Tofauti na wakristo baadhi wanavyozani kuwa majuma hayo sabini yote yamekwisha timia, jibu ni hapana, majuma hayo bado hayajatimia yote bali ni majuma sitina na tisa tu. Ili tuelewe vizuri hebu tusome kidogo
Danieli 9:23 Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya.
24 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.
25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.
26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.
27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
Tukisoma hapo maandiko yanasema kuwa, majuma hayo yaliamriwa kwa lengo la
a/ kukomesha makosa
b/ kuishilishia dhambi
c/ kufanya upatanisho kwaajiri ya uovu
d/ kuleta haki ya milele
e/ kutia muhuri maono ya unabii
f/ kumtia mafuta aliye mtakatifu
Sasa baadhi ya hayo yamekwisha timia, mfano wa hilo ni la kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu (masihi) lakini mengine bado hayajatimia kwa ukamilifu kwa mfano lile la kufanya upatanisho kwaajiri ya uovu kwa wana wa Israel ambalo litakuja kufanyika baadae pale wayahudi watakapo mwamini masihi wao kwa mahubiri ya mashahidi wawili tunaowasoma katika kitabu cha ufunuo
Lakini pia jiulize kuwa, lengo lingine la majuma haya likikua ni KUKOMESHA DHAMBI, sasa kama majuma haya yangekuwa yameshatimia basi ni wazi kuwa sasa hivi dhambi isingekuwapo duniani, kwahiyo dhana ya kusema kuwa majuma haya yameshatimia ni potofu
Lakini pia ukisoma mstari wa 27 unasema
Danieli 9:27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
Kwamantiki hii tukisema kuwa majuma haya yameshatimia basi ni wazi kuwa hata hii ghadhabu ya Mungu imekwisha kumwagwa kitiu ambacho sio sahihi.
Ndugu yangu hizi ni siku za mwisho na kuna mafundisho mengi sana ya mashetani na roho zidanganyazo kama maandiko yalivyotabiri, hivyo kuwa makini na wewe usiwe mmoja wapo wa wanao sikiliza roho zidanganyazo
1 Timotheo 4:1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
Bwana akubariki. Shalom