JE UTASI NI UGONJWA GANI? (Marko 7:32).

Maswali ya Biblia No Comments

JIBU..

Kuna utofauti kati ya haya Maneno mawili, Utasi na Utasa.. tasa ni ile hali ya mtu kutokuwa na uwezo wa kuzaa au kuzalisha,kwa mwanamke au mwanaume lakini utasi ni hali ya ulimi kuwa mzito, wengi wenye changamoto ya utasi wanakuwa hawawezi kuongea Katika ufanisi au kuyatamka Maneno vizuri, na huwa tatizo la utasi mtu huzaliwa nalo..

Ugonjwa hu umetajwa sehemu moja kwenye maandiko.. Tusome..

Marko 7:32-35

[32]Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono.

[33]Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi,

[34]akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka.

[35]Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri..

Bwana Yesu bado ni yule yule, alitenda kwa mtu huyu na kumfanya aongee tena, Kumbuka ana uwezo wa kutenda zaidi na kwako,kukuponya na zaidi pia ana uwezo wa kufanya, mamlaka hiyo anayo…

Yeye anaponya magonjwa yote, lakini Uponyaji mkubwa ambao Bwana anautoa kwetu ni UPONYAJI WA ROHO ZETU, ni muujiza mkubwa Bwana anatufanyia pale tunapomwani na kuja kwake…

Tukimwamini Bwana Yesu anatuponya na kutuepusha na mauti ya rohoni, tunaepukana na ghababu na mapigo ya Mungu Katika ulimwengu kwa watenda maovu..

Na wewe je umeupokea Uponyaji huu leo, ni rahisi sana, Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa na kubatizwa ubatizo sahihi,upokee Roho Mtakatifu na kupata ondoleo la dhambi, hapo umeponyeka Kweli kweli..

Maran atha

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *