KAFIRI NI MTU GANI?

  Maswali ya Biblia

Kafiri ni mtu ambaye haamini imani fulani. Makafiri ni wale ambao hawaamini kwamba Kristo alikuja na kufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, hawa hawana tofauti sana na wapagani.

Mtu yeyote asiyeshika njia za Bwana Yesu Kristo(neema) na kumkana, mtu huyo ni kafiri…

Yuda 1:14 “Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo”

Kwahiyo kafiri ni nani?

…Jibu: Mtu yeyote asiyempenda Bwana YESU huyo ni kafiri, na tena Biblia inasema Amelaaniwa

2Wakorintho 16:22 “Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha”. Ili kuepuka kuwa kafiri, ni lazima mtu akiri Yesu Kristo, na kumwamini, na kumpa maisha yake.

Yohana 3:18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.

20 Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.

(Makafiri) Wasioamini Yesu Kristo(neno la Mungu) hawatarithi uzima wa milele kwa sababu hawajamwamini Mwana wa pekee wa Mungu, Yesu Kristo kwa kumfanya Mungu ni muongo bali Shetani wamemwamini ni sawa na Adamu na Eva walivyo danganyika wakajikuta wanapoteza uzima wa milele na na kusababisha Kifo kumtawala mwanadamu.

Kama ujampokea Kristo(kuokoka) kwa moyo wako amua leo Bwana anakupenda sana. wasiliana nasi kwa namba hizi: +255693036618 au +255789001312.

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

LEAVE A COMMENT