JE MUNGU ANAJUTA?

  Maswali ya Biblia

Kutokana na vifungu hivi je Mungu anajuta?

Hesabu 23:19
[19]Mungu si mtu, aseme uongo;
Wala si mwanadamu, ajute;
Iwapo amesema, hatalitenda?
Iwapo amenena, hatalifikiliza?

1 Samweli 15:11
[11]Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha.

Ukitazama vifungu hivyo ni kama vinakinzana, utaona hapo kwenye kitabu cha hesabu kinasema yeye si mwanadamu hata AJUTE, alafu tena katika 1 Samweli inasema Mungu ANAJUTA

Je ni kweli Mungu anajuta?

Ukweli ni kwamba MUNGU wetu hawezi kujuta hata siku moja, isipokuwa sasa huwa kuna wakati anajiweka katika mazingira ya kibinadamu ili kutufanya wanadamu nasi tuzielewe hisia zake vyema .

Ndiyo maana tukisoma kitabu cha mwanzo Mungu anazionyesha kazi zake kama hazijakamilika vile, na kutumia neno hili SI VEMA “mtu huyu aishi peke yake nitamfanyia msaidizi, hapo Mungu anasema hivyo kana kwamba hakuliona hilo tangu mwanzo, lakini ukisoma mwanzo ni mwa kitabu cha mwanzo 1:27 inasema tayari alimuumba mwanaume na mwanamke katika mwanzo wa uumbaji wake, lakini katika utekelezaji anajifanya kama kasahau, ndipo hapo anakuja kumuumba mwanamke baadaye
Soma mwanzo 2:8

Hiyo ndiyo tabia ya Mungu kuna wakati mwingine anajiweka hivyo ili kutufundisha na sisi jambo

Na si tu katika uumbaji wake, kuna wakati mwingine anajiweka kama hana mashauri yaliyo bora kumzidi mwanadamu
Jambo hili tunaliona kwa Musa kule jagwani tunaona Musa alimshauri Mungu aghahiri mabaya kwa wana wa Israeli, lakini hii haimaanishi kuwa mashauri yetu ni bora zaidi ya Mungu
Somo kutoka 32:9-14

Na hapo anaposema Yeye si mwanadamu hata ajute inamaanisha kuwa mipango yake yote tayari anaifahamu tangu mwanzo, anajua kabisa mwisho wa jambo litaishia pazuri au pabaya, jambo hili hata kwa shetani si kwamba Mungu hakujua kwamba mwisho wake utakuwa mbaya na hata kwa malaika aliowaumba si kwamba hakujua kwamba baadhi yao wataasi na kuja kuwapoteza wanadamu wengi hilo alijua kabisa, … Na ndiyo maana aliwaumba hivyo hivyo

Tambua hili hata sasa Mungu anajua kabisa mwisho wa kila mwanadamu atakapoishia, ndiyo maana hata kwenye hiyo habari ya sauli si kwamba Mungu hakujua mwisho wake alifahamu kwamba atabadilika, lakini alimpa ufalme

Hata kwetu pia, ukweli ni kwamba lazima tujue , Mungu kutupa jambo fulani ambalo linakufanya upate sifa leo, haimaanishi hiyo ndiyo tiketi ambayo itakufanya kwenda mbinguni moja kwa moja, Mungu kukupa hiyo karama au huduma na kuwaacha wengine haimaanishi wewe ndiyo kipenzi cha Bwana, hata ukifanya dhambi Bwana atakusitiri ile siku ya hukumu, kwa sababu tu alikutia mafuta, usidanganyike

Yaani kama ulienda nje ya maagizo ya Mungu jua kabisa Bwana hatakubaliana nawe

Mathayo 7:21-23
[21]Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

[22]Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
[23]Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Swali ni je…umempa Kristo maisha yako na kusimama kweli kweli? Unahabari kuwa Karama pekee sio uthibitisho kuwa Mungu yupo na wewe? Wakati wowote anaweza kujutia na kughahiri huo wito wako, aliokupa kama unasua sua

Kama hujasimama imara, fanya hivyo sasa. Mgeukie muumba wako kwa kumaanisha kwasababu, kumbuka hizi ni siku za mwisho na Kristo yupo mlangoni kurudi

Bwana akubariki.

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

LEAVE A COMMENT