Uasherati. Ni kitendo cha kufanya tendo la ndoa kwa makubaliano ya hiari kwa watu wawili mwanamke na mwanamume ingali bado hawajaowana. Neno hili alilizungumza Bwana wetu Yesu Kristo.
Mathayo 5:32
[32]lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya UASHERATI, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.”
Hivyo ikiwa umewahi kufanya ngono kabla ya kuoa ama kuolewa huo ni uasherati.
Uzinzi. Ni kitendo cha kufanya tendo la ndoa kati ya mtu alieowa/kuolewa na mtu ambae hajao/hajaolewa.
Kitendo cha kutoka nje ya ndoa(kutokuwa mwaminifu katika ndoa) huo ni uzinzi.
Aina kuu Tatu za uzinzi.
1. Umeowa/ kuolewa na ukafanya tendo la ndoa na mtu alieowa/kuolewa.
2.Hujaoa/kujaolewa ukafanya tendo la ndoa na mtu ambae yupo katika ndoa.
3.upo katika ndoa na ukafanya tendo la ndoa na mtu ambae yupo pia katika ndoa. Ambae si mwezi wako yaani hujafunga nae ndoa.
Biblia imeeleza katika Agano la Kale na Agano Jipya Mungu ametumia neno Uasherati ambao pia ulikuwa ukimaanisha Uzinzi.
Katika agano la kale wana wa Israeli walikuwa ni wazinifu katika roho yaani walikuwa wakiwatumikia miungu mingine kama baali nk na kumuacha Mungu mwenyewe muumba wa mbingu na nchi(Elohim).
Ezekieli 22:11
[11]Na mtu mmoja amefanya chukizo pamoja na mke wa jirani yake; na mtu mwingine amemharibu mke wa mwanawe kwa UASHERATI; na mtu mwingine ndani yako amemfanyia nguvu umbu lake, binti ya babaye.”
Pia Soma Ufunuo 17:1-5, 2 Mambo ya nyakati 21:10-14.
Basi ikiwa uko katika ndoa basi I iheshimu ndoa yako, Epuka kutoka nje ya ndoa na wewe ambae hujaoa wala hujaolewa usiwe na papara tulia wakati wako ufike usifanye ngono na mtu ambae hamjaowana.
Wala usikubali kamwe kuwa mzinzi kwa kuchukua mke wa mtu ama mume wa mtu epuka kwani hakika madhara yake ni Makubwa sana Epuka tamaa.
Shalom.
Ubarikiwe.Tafadhali Shirikisha. na kwa wengine..
NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618