Kuzumbua Ni nini kama inavyotumika kwenye biblia.(Walawi 6:3)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Kuzumbua maana yake ni kuwa na uwezo kupata kitu Fulani, hususani kile Cha lazima.

Kwamfano Unaweza kusema;

Namshkuru Mungu nimezumbua kile kitambulisho changu kilichopotea siku nyingi.

Maana yake nimekipata kitambulisho changu.

Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi kwenye biblia

Mambo ya Walawi 6:1-7

[1]BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

[2]Mtu awaye yote akifanya dhambi, na kuasi juu ya BWANA, akamdanganya mwenziwe katika jambo la amana, au la mapatano, au la kunyang’anya, au kumwonea mwenziwe;

[3]au kuzumbua kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo; katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo;

[4]ndipo itakapokuwa, akiwa amefanya dhambi, na kupata hatia, atarudisha hicho alichokipata kwa kunyang’anya, au kitu kile alichokipata kwa kuonea, au ile amana aliyowekewa, au kitu kile kilichopotea alichokizumbua yeye,

[5]au kitu cho chote ambacho amekiapia uongo; atakirudisha hata kwa utimilifu wake, kisha ataongeza na sehemu ya tano zaidi juu yake; naye atampa huyo mwenyewe, siku hiyo ambayo atakapohukumiwa kuwa mwenye hatia.

[6]Kisha ataleta sadaka yake ya hatia kwa BWANA, ni kondoo mume wa katika kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, na kumpa kuhani;

[7]na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, naye atasamehewa; katika jambo lo lote alifanyalo hata akapata kuwa mwenye hatia kwalo.

Vifungu hivyo vinatuonyesha kuwa ni  dhambi kuchukua kitu Cha mtu alichokipoteza na kukiifanya kama ni chako, kisa hujakiiba. Kwamfano umeokota pochi yenye pesa, Kisha ukaona muhusika anaiulizia, halafu na wewe ukakaa kimya kana kwamba hufahamu lolote, sasa hiyo ni dhambi…lakini kama umekiokota halafu muhusika hajulikani hata baada ya kuulizia..hapo huna hatia.

Na adhabu yake ulipogundulika ilikuwa unalipa mara 5 ya hicho ulichokiiba.

Hata sasa, adhabu hii IPO Rohoni Unaweza usionekane na mwanadamu lakini Mungu anakuona, Mungu atafanya ukirejeshee tu mara 5. Hivyo Mahali popote upatapo kitu ambacho sio Mali Yako ni hekima uulize kwanza, Umpate mhusika, pale utakapomkosa ndio ukifanye ni chako. Muuza duka, kakuuzia bidhaa, kisha akakuzidishia chenji, hupaswi kukaa kimya, mrejeshee fedha yake, kwasababu ndio kwa ajili ya hiyo ndio anategemea faida yake. 

Bwana akubariki.

Je! Kristo yupo moyoni mwako? Je una habari kuwa Unyakuo wa kanisa upo karibu? Umejiandaaje kumlaki Bwana Yesu mawinguni atakaporudi? Akikukuta katika hali ya dhambi utajibu nini, Kama bado upo nje ya Kristo nafasi ndio hii sasa..Ikiwa umedhamiria moyoni mwako kufanya hivyo leo, basi fungua hapa ili kupata mwongozo huo wa kumkaribisha Yesu maishani mwako.. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Shalom

Kwa mawasiliana/ maswali/ Ubatizo. piga namba hizi +255693036618/+255789001312

Mada Nyinginezo

Mauti na uzima huwa katika uweza wa ulimi.

KWA WINGI WA WASHAURI HUJA WOKOVU.

MAHANAIMU (Jeshi la Mungu)!.

SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.

Pango la Makpela

Rudi Nyumbani

LEAVE A COMMENT