UNADHANI WAKATI WAKO SAHIHI WA KUMTII MUNGU BADO?

Katika vitu ambavyo watu wengi wameshindwa kuelewa ni hapa, kujua wakati na majira sahihi katika maisha yao juu ya Mungu, na hapa ndipo shetani amewekeza nguvu kubwa sana ili awanase wengi, na ndio maana siajabu leo hii mtu akihubiriwa habari njema za wokovu, anakwambia wakati wangu bado, au atakwambia siwezi kumdanganya Mungu kumpa maisha yangu sasa hivi nikiwa kijana, au mwengine atakwambia mpaka nitakapoona kiu yangu ya uzinzi imekata ndipo nitarejea kwa Mungu.


Lakini anasahau kuwa, wakati yeye anapanga Muda wake, na Mungu Naye Ameshampangia hitimisho la uhai wake, wakati wewe unasema huu sio muda sahihi, kumbe Mungu anatazamia kitu fulani kutoka kwako wakati huo huo, mfano mzuri ni pale Bwana alipotazamia matunda kutoka kwa mtu (tini), ambao haukuwa wakati wake.

[Marko 11:12] Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa.

[13] Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.

[14] Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia.

Umeona hapo? Bwana Yesu Alifahamu kabisa kuwa, ule wakati haukuwa wakati wa tini kutoa matunda lakini Yeye alienda kutafuta matunda hapo. (Mtini ni mti unao zaa matunda ya tini)


Sasa unaweza kujiuliza swali hili, ikiwa haukuwa ni wakati wa tini kutoa matunda yake, ni kwanini basi Bwana Yesu alienda kutafuta matunda hapo, je kulikuwa na jambo gani Bwana alilohitaji tujifunze?


Jibu ni kwamba, kama vile ambavyo wewe unafikili kuwa wakati sahihi labda mpaka nikioa au kuowa, au unafikili kuwa wakati sahihi ni mpaka pale nitakapokuwa mzee, au mpaka nitakapo pata pesa nyingi au kazi, ndipo umgeukia Mungu na kumzaliq matunda, kumbe Bwana Yeye hatazami hivyo, Yeye anatazamia matunda muda wote, hivyo ikiwa unasubiri au unasema kesho ndio nitachukua maamuzi, basi tambua kuwa, Bwana anakuja kutafuta matunda sasa hivi na sio kesho au mwakani.

Bwana akubariki, Shalom.


Mada zinginezo:

MADHARA YA KULISIKIA NENO LA MUNGU NA KUTOWAZA  KUCHUKUA UAMUZI WO WOTE ULE WA KULIFANYIA KAZI (KULITII)


KAMA MWANAFUNZI WA YESU KRISTO, KUWA NA TABIA WALIYOKUWA NAYO WANAFUNZI WA YESU KRISTO KATIKA MAANDIKO.


UMEFUNGULIWA KAMA BARABA?


Je! Ni kweli Ibrahimu na sara walikuwa ni ndugu wa baba mmoja? (Mwanzo 20:12), Na kama ni ndio, kwanini Mungu aliruhusu ndugu hao kuoana?


KWA MAANA ISRAELI AMETENDA KWA UKAIDI, KAMA NDAMA MKAIDI; SASA JE! BWANA ATAWALISHA KAMA MWANA KONDOO KATIKA MAHALI PENYE NAFASI?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *