KAMA MWANAFUNZI WA YESU KRISTO, KUWA NA TABIA WALIYOKUWA NAYO WANAFUNZI WA YESU KRISTO KATIKA MAANDIKO.

Kama Wewe ni Mwanafunzi na mfuasi wa Yesu Kristo (uliyetubu dhambi zako na kuamua kumfuata na kumuamini Yesu Kristo sawasawa na maandiko kama Yeye mwenyewe alivyosema), basi, huna budi kujifunza na kuwa na tabii ambayo inaoneshwa katika maandiko matakatifu na wanafunzi wa Yesu Kristo wakati alipokuwa duniani, Ni kwanini? kwa sababu, tabia hiyo waliyokuwa nayo wanafunzi wa Yesu Kristo haikuandikwa bure bure tu bila sababu yo yote ya msingi, Bali iliandikwa ili kuwa msaada kwa yo yote yule anayemfuata Kristo, kwamba anapaswa awe nayo ili kuhakiki wokovu wake.


Sasa kabla hatujaitaja tabia hiyo moja kwa moja, hebu tusome vifungu vifuatavyo kwanza vya maandiko (ZINGATIA MANENO YALIYOANDIKWA KWA HERUFI KUBWA).

[Matayo 17:10] WANAFUNZI WAKE WAKAMWULIZA, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? 

Soma tena

[Marko 7:17] Hata alipoingia nyumbani, ameuacha mkutano, WANAFUNZI WAKE WAKAMWULIZA habari za ule mfano. 

Soma tena 

[Marko 9:28] Hata alipoingia nyumbani, WANAFUNZI WAKE WAKAMWULIZA kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa? 

Soma tena 

[Luka 8:9] WANAFUNZI WAKE WAKAMWULIZA Maana yake nini mfano huo? 

Soma tena

[Yohana 9:2] WANAFUNZI WAKE WAKAMWULIZA wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? 

Umeona hapo tabia waliyokuwa nayo wanafunzi wa Yesu Kristo? Kwamba, walikuwa ni watu wa kuuliza maswali, na tena, pale ambapo hawakuelewa au pale ambapo walipoona maandiko yanasema hivi na hivi hivyo kutaka kujua maelezo zaidi


Hii inafundisha nini? 

Hii inatufundisha kuwa, ikiwa Yesu Kristo, Aliye Mtume na Kuhani Mkuu (Waebrania 3:1), mchungaji Mkuu (1 Petro 5:4), na nabii Mkuu (Luka 7:16), na Mwalimu Mkuu, aliulizwa maswali na wanafunzi wake, je! Si zaidi sana mtume wako au nabii wako na mchungaji wako kuulizwa maswali na wewe?


Hivyo basi, hata sasa na wewe uliyemwamini Yesu Kristo, huna budi kuwa na tabia hii ndani yako kwa kumuuliza maswali kiongozi wako (awe askofu, mchungaji, mwalimu, mtume n.k), kwa lengo la kuhakiki wokovu wako na imani yako kwa Yesu Kristo, kwamba je! Inaendana na maandiko matakatifu? (biblia), au ni mawazo na mitazamo yake kiongozi wako? Na kama sivyo, basi, kiongozi wako anakudanganya na kukukosesha, na mwisho wako ni kuwa, utaangamia kama maandiko yanavyosema katika..[Isaya 9:16]

[Isaya 9:16] Kwa maana WAWAONGOZAO watu hawa NDIO WAWAKOSESHAONA HAO WALIOONGOZWA NA WATU HAO WAMEANGAMIA

Hivyo Muulize mchungaji wako maswali na wala usiogope, Muulize mtume wako na mwalimu wako maswali na wala usiogope, ikiwa Mchungaji Mkuu, Kuhani Mkuu, nabii Mkuu, mtume Mkuu aliulizwa maswali Kwanini wewe uogope kumuuliza mchungaji wako?


Muulize Mbona sisi tunafanya hivi na maandiko yanasema hivi? Muulize Mbona sisi tunafanya hivi na biblia haisemi hivi na tena inakataza kufanya hivi? Muulize mbona biblia inasema Mariamu amebarikiwa KATIKA wanawake lakini wewe unasema KULIKO WANAWAKE WOTE?

[Luka 1:42] akapaza sauti kwa nguvu akasema, UMEBARIKIWA WEWE KATIKA WANAWAKE, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. 

Hivyo kuwa na tabia hiyo ndani yako ya kuuliza maswali kama wanafunzi walivyokuwa kwa lengo la kuhakiki imani yako kwa Yesu Kristo.

Tafadhari washirikishe kanisa la Kristo ujumbe huu.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

JIFUNZE TABIA HII KUTOKA KWA MITUME ANDREA NA FILIPO.


Jifunze tabia hii kutoka kwa mtume Paulo.


Nini maana ya mstari huu “na mtu mmoja ajengapo ukuta, tazama, waupaka chokaa isiyokorongwa vema” (Ezekieli 13:10)


BINTI YA KUHANI YE YOTE ATAKAPOJITIA UNAJISI KWA UKAHABA, AMEMTIA UNAJISI BABA YAKE, ATACHOMWA MOTO 


NI BWANA GANI HUYO AMBAYE MANABII WALITABIRI KWA JINA LAKE NA KUTESWA KWA AJILI YAKE?

2 thoughts on - KAMA MWANAFUNZI WA YESU KRISTO, KUWA NA TABIA WALIYOKUWA NAYO WANAFUNZI WA YESU KRISTO KATIKA MAANDIKO.
  1. asante sana ila kama upande wangu nawezapenda kuuliza maswali maana kwanza atubatizi ubatizo sahihi na wakati wa meza tunatumia juis badala ya divai, sasa ninapouliza maswali kama nahayo yanaleta shida hata kwangu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *