NI BWANA GANI HUYO AMBAYE MANABII WALITABIRI KWA JINA LAKE NA KUTESWA KWA AJILI YAKE?

  Mungu, Uncategorized


SWALI: Katika agano la kale tunaona manabii walipotabiri, walitabiri kwa jina la Bwana, na tena si hivyo tu, lakini pia waliteswa, walinusurika kuuwawa na wengine hata kuuwawa kabisa kwa ajili ya Bwana huyo huyo ambaye walitabiri kwa jina lake, kwamfano nabii Uria Mwana wa Shemaya, ambaye baada ya kutabiri kwa jina la Bwana juu ya uovu ujao katika mji wa Yerusalemu, mfale Yehoyakimu alimwua kwa upanga.

Yeremia 26:20 Tena, kulikuwa na mtu ALIYETABIRI KATIKA JINA LA BWANA, Uria, mwana wa Shemaya, wa Kiriath-Yearimu; yeye naye alitabiri juu ya mji huu, na juu ya nchi hii, sawasawa na maneno yote ya Yeremia; 

21 na Yehoyakimu, mfalme, na mashujaa wake wote, na wakuu wake wote, waliposikia maneno yake, mfalme akataka kumwua; lakini Uria alipopata habari, aliogopa, akakimbia akaenda Misri.

22 Basi, mfalme Yehoyakimu akatuma watu waende Misri, Elnathani, mwana wa Akbori, na watu wengine pamoja naye, kwenda Misri; 

23 wakamtoa Uria katika Misri, wakamleta kwa Yehoyakimu, mfalme; NAYE AKAMWUA KWA UPANGA, akamtupa yule maiti katika makaburi ya watu wasio na cheo. 

Swali je! Ni Bwana gani huyo ambaye manabii walitabiri kwa jina Lake na kuteswa kwa ajili yake?


JIBU: Bwana ambaye manabii walitabiri na kuteswa kwa ajili Yake alikuwa ni Mungu wa Israeli, Mwokozi, Yehova, Bwana wa majeshi.

Isaya 43:3 Maana mimi ni BWANA, MUNGU WAKO; Mtakatifu wa Israeli, MWOKOZI WAKO, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako. 

Sasa ili tumuelewe ni nani Huyo ambaye manabii waliteswa na kuuwawa kwa ajili yake tusome vifungu vifuatavyo (ZINGATIA MANENO YALIYOANDIKWA KWA HERUFI KUBWA).

Matayo 5:11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, KWA AJILI YANGU.

12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; KWA MAANA NDIVYO WALIVYOWAUDHI MANABII WALIOKUWA KABLA YENU

Umeona hapo? Manabii waliokuwa kabla yetu waliudhiwa na kuteswa kwa ajili ya Yesu Kristo..Hivyo basi, Bwana (ambaye ni Mungu wa Israeli, Mfalme Mkuu, Bwana wa majeshi, n.k), ambaye manabii waliteswa na kuudhiwa kwa ajili Yake ni Yesu Kristo, huyo Ndiye Mfalme na Bwana wa majeshi.

Zekaria 14:16 Hata itakuwa, ya kwamba kila mtu aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja kupigana na Yerusalemu, atakwea mwaka baada ya mwaka ILI KUMWABUDU MFALME, BWANA WA MAJESHI, na kuishika sikukuu ya Vibanda. 

Na pia ili tuelewe ni Bwana gani Ambaye manabii walitabiri kwa jina Lake, tusome kifungu kifuatacho katika maandiko (ZINGATIA MANENO YALIYOANDIKWA KWA HERUFI KUBWA).

Matayo 7:22 Wengi wataniambia siku ile, BWANA, BWANA, HATUKUFANYA UNABII KWA JINA LAKO, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 

Umeona na hapo? Kumbe Bwana Ambaye manabii wake na wa uongo (kama Hanania) waliotabiri kwa jina lake wakati ule ni Yesu Kristo, na hata sasa manabii wote wa kweli na wa uongo wanatabiri kwa jina la Bwana huyo huyo (ijapokuwa jina hilo halikufunuliwa kwa wakati huo).


Hivyo kwa kuhitimisha ni kwamba, Yesu Kristo Ndiye Bwana ambaye manabii walitabiri, kuteswa na kuuwawa kwa ajili yake, Zekaria bin Barakia alipigwa mawe na kuuwawa kwa ajili ya Bwana ambaye ni Yesu Kristo, Stephano alipigwa mawe na kuuwawa kwa ajili ya Bwana ambaye ni Yesu Kristo, nabii Uria aliuwawa kwa upanga kwa ajili ya Bwana ambaye ni Yesu Kristo, mtume Yakobo mwana wa Zebedayo aliuwawa kwa upanga kwa ajili ya Bwana ambaye ni Yesu Kristo, nabii Mikaya alifungwa gerezani kwa ajili ya Bwana ambaye ni Yesu Kristo, nabii Sila na mtume Paulo walifungwa gerezani kwa ajili ya Bwana ambaye ni Yesu Kristo, na mtu Yoyote Yule uliyemwamwamini Yesu Kristo ategemea kupitia mambo yanayofanana na hayo katika safari yake ya hapa duniani maana imeandikwa.

Wafilipi 1:29 Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, SI KUAMINI TU, ILA NA KUTESWA KWA AJILI YAKE

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zingineno:

JE! KAMA BWANA YESU NDIYE MUNGU, KULE MLIMANI ALIENDA KUMUOMBA NANI? (Luka 6:12)


DAIMA HUWAAMBIA WAO WANAONIDHARAU, BWANA AMESEMA, MTAKUWA NA AMANI.


Bwana alimaanisha nini aliposema “Heri ayawe yote asiyechukizwa nami?” (Mathayo 11:6)


BASI ‘BWANA’ NDIYE ROHO.


Kwanini Bwana Yesu alijeruhiwa ubavuni pale msalabani?

LEAVE A COMMENT